Mh.Lowassa asema ameshakamilisha mipango na taratibu za kuondoa kero za watanzania
Mgombe urais wa vyama vinavyounda UKAWA Mh Edward Lowassa ameingia jijini Dar es Salaam kwa kishindo na kunadi sera katika jimbo la Kawe na Kibamba na amesema ameshakamilisha mipango na taratibu za kuondoa kero za watanzania anachosubiri ni ridhaa yao ya kumchagua kuwa rais ili aanze utekelezaji wa kuthibitisha ahadi zake kwa vitendo.
Baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunju ambavyo vilifurika
maelfu ya wananchi wakimsubiri, Mh Lowassa amesema anaifahamu Tanzania
vizuri na matatizo ya wananchi wakiwemo wa jiji la Dar es Salaam na
amewaomba watanzania wampime kwa kumpa nafasi ili waone Tanzania mpya
ambayo haijawahi kutokea tangu uhuru.
Aidha Mh Lowassa amesema akiwa rais atahakikisha kuwa wawekezaji
wote wanaingia ubia na watanzania ili kuleta usawa wa kunufaika na
rasilimali za nchina kuhusu wasiwasi wa kuibiwa kura amesema hilo
haliwezekani kwani wapo vijana wa kutosha kulinda kura na ni jambo
linalowezekana.
Awali mwenyekiti wa Chadema Mh Freeman Mbowe na baadhi ya wagombea
ubunge akiwemo Halima Mdee wamewataka wananchi kupuuza njama za CCM za
kuwasakama viongozi wa UKAWA na watanzania wengine wanaounga mkono
mabadiliko.
Aliyekuwa waziri mkuu Mh Fredirick Sumaye ambaye kwa sasa amejuinga
na UKAWA amewataka watanzania kutokatishwa tamaa na wanaoendelea
kuwasakama wananchi wanaotumia haki yao ya kutaka mabadiliko kwani
wanaongeza chachu ya mabadiliko.
Mchaka mchaka wa vuguvugu la mabadiliko unaoongozwa na Mh Lowassa viongozi wengine wa UKAWA unaelekea katika mkoa wa Morogoro.


Post a Comment