Mgombea urais Chadema asema anajua vizuri mahitaji na kero za watanzania.
Mgombea urais wa vyama vinavyounda UKAWA Mh Edward Lowassa aendelea
na kampeni za kunadi sera zilizoko kwenye ilani ya UKAWA katika mkoa wa
Rukwa na amewaomba watanzania kumpa dhamana ya kuleta mabadiliko ya
kweli kwani uwezo huo anao na anachohitaji ni ushirikiano wao.
Mh Lowassa akiambatana na viongozi na wanachama wa UKAWA baada ya
kupata mapokezi makubwa ya aliyoanzia kwenye uwanja wa ndege wa
Sumbawanga anazungumza na maelfu ya wananchi walijitokeza amesema anajua
vizuri mahitaji na kero za watanzania na mahitaji nafasi ya kuziondoa.
Kuhusu tuhuma na hatua ya katibu wa Chadema Mh Wilbroad Slaa ya
kujiengua mwenyekiti wa Chadema Mh Freeman Mbowe amesema chama kiko
imara kwani ni sio mali ya mtu mmoja ni mali ya watanzania wote na
hakuna muda wa kupoteza kwani watanzania wanahitaji na wako tayari kwa
mabadiliko.
Mgombea ubunge wa jimbo la Sumbawanga pamoja na kuwaomba wananchi
kumchagu Mh Lowassa na viongozi wengine wa UKAWA ili waweze kuondoa kero
za muda mrefu ikiwemo ya maji na huduma zingine za kijamii.
Post a Comment