Lowassa, Magufuli wavunja kambi ya Yanga Bagamoyo
Nassor Gallu,
Dar es Salaam
ILE kambi ya Yanga SC, iliyotarajiwa kuwekwa Bagamoyo kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu Bara kuanzia Jumamosi hii, imelazimika kuvunjwa chanzo kikiwa ni wagombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), John Pombe Magufuli na yule wa Chadema kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.

Yanga iliyo chini ya Mholanzi, Hans van Der Pluijm, ilipanga kuanza kambi hiyo leo na kujipanga zaidi kwa ajili ya mchezo wake wa kwanza dhidi ya Coastal Union ya Tanga, Jumapili hii lakini sasa mpango huo ‘umefukiwa’ na sasa timu hiyo itabaki jijini Dar mpaka ligi hiyo itakapoanza.
Imeelezwa kuwa kila kitu kilikuwa kimepangwa sawia lakini ghafla baada ya Lowassa kurejea Dar akitokea mikoani kwa ajili ya kuja kupiga kampeni, uongozi wa Yanga ukabaini kuwa hilo linaweza kuondoa umakini wa kujikita na maandalizi yao na badala yake wakahamia kwenye kufuatilia siasa.
Hiyo imekuja baada ya kuvuja kwa ratiba inayoeleza kuwa Lowassa anaweza akatua Bagamoyo hivi karibuni kwa ajili ya kwenda kunadi sera zake, hivyo Yanga ikaamua kuuepuka mgongano huo ikiwemo pia kuingiliana katika suala la utumiaji wa viwanja.
Championi Jumatano limezungumza na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Yanga, Jerry Muro na kubainisha kwamba wamebadili upepo ghafla kutokana na wimbi la kisiasa ambalo sasa limehamia katika ukanda huo, huku viwanja na sehemu nyingi za wazi zikitumiwa zaidi na wanasiasa katika kunadi sera zao ili kuwashawishi wananchi wawapigie kura katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.

“Kambi ya Bagamoyo tumeivunja, tumeamua kubaki hapahapa Dar kwa ajili ya maandalizi ya siku chache kabla ya ligi kuanza. Kweli tulipanga kwenda Bagamoyo kesho (leo), lakini tukatafakari hizi ishu za siasa tukaona zitatupotezea utulivu na pia viwanja vingi vinatumika wakati huu, hivyo tunaweza kupata changamoto.
“Lakini kingine ni kwamba tuliamua tukae Bagamoyo kisha tufanye mazoezi Dar pale kwenye Uwanja wa Boko, bado tukaona ni kujitesa na kuwachosha wachezaji. Kwa kuliangalia hilo, tumeamua kuendelea na programu zetu tukiwa Dar.
“Tutaendelea kujifua palepale kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Polisi kwa ajili ya sababu za kiufundi tayari kwa kampeni ya kutetea ubingwa na kushiriki vyema michuano ya kimataifa. Kama unavyojua sisi ni wa kimataifa,” alifafanua Muro aliyetoswa kwenye kura za maoni za kuwania ubunge katika Jimbo la Kawe, Dar kupitia CCM.

Post a Comment