Kiongozi wa FDLR afungwa miaka 13 Ujerumani
Mahakama moja ya Ujerumani
imewahukumu viongozi wawili wa waasi nchini Rwanda kwa kupanga njama za
kushambulia raia katika jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Ignace
Murwanashyaka na Straton Musoni wanatuhumiwa kwa kuwaagiza wapiganaji
kufanya mauaji ya halaiki pamoja na ubakaji kati ya mwaka 2008 na 2009.Hatua hiyo ilionekana kama ushindi dhidi ya waasi waliotekeleza uhalifu nchini Rwanda.
Murwanashyaka,ambaye ni kiongozi wa kikosi cha FDLR alipewa hukumu ya miaka 13 huku Musoni ambaye ni naibu wake akihukumiwa mika 8 jela.Hatahivyo Musoni ameachiliwa huru kutokana na miaka aliyokuwa akizuiliwa.
Wawili hao waliokamatwa ,mwaka 2009 wamekuwa wakiishi nchini Ujerumani tangu mapema miaka 1990 na kutoka huko walipanga mashambulizi dhidi ya raia mashariki mwa Congo.
Walishtumiwa kwamba waliagiza mauaji ya watu kwa kukataa kushirikiana na FDLR.
CHANZO; BBC SWAHILI

Post a Comment