Singidani (A Story From My Heart) - 6

ILIPOISHIA...
“Lakini nikimkosa usiku huu, sitaeleweka. Anaweza kuniona sijakamilika,” akazidi kuwaza Chris.
SASA ENDELEA...

HRIS aliinuka kitandani lakini akiwa
tayari ameshainuka, akajishangaa maana hakujua aliinuka ili kufanya nini!
Hakutaka kuonekana kama alikuwa hajui cha kufanya.
Akamwangalia Laura kwa jicho lililojaa ubembe, kisha akamsogelea na kukaa kwenye sofa kubwa lililotosha kukaliwa na watu wawili tu, akapiga magoti chini yake.

Bado hakujua alichotaka kumwambia.
Bahati nzuri, Chris alikuwa na utajiri wa maneno kwa hiyo haikumpa shida sana.
Laura akashangazwa na namna Chris alivyopiga magoti mbele yake.
“Sikia nikuambie Laura. Mimi ni mwanaume wa tofauti sana. Mara zote nimekuwa mkweli na ninayeheshimu hisia zangu. Kila kinachotoka kinywani mwangu, huwa yakinifu kabisa,” akasema Chris, kisha akatulia kidogo.

Ni kama alikuwa akifikiria jambo.
Kichwani Laura akaanza kuona hisia za mapenzi kutoka kwa Chris kwenda kwake.
Pamoja na kwamba alikuwa ameonja kidogo kilevi, hakuwa tayari kumpa Chris mwili
wake kwa sababu tu ni staa wa filamu.
Alifika pale hotelini kwa heshima tu. Alimwamini ghafla sana. Hakutegemea kama angetongozwa na hata kama angetongozwa, hakuwa tayari kujiachia kwa siku hiyohiyo!

“Ameanza....nilijua tu. Wanaume
bwana!” akawaza Laura.
“Lakini hapati kitu hapa,” akawaza tena.
Chris akaendelea: “Shika haya maneno yangu Laura. Nayaona maisha yako miaka miwili ijayo, jinsi utakavyokuwa staa na maisha yako yatakavyobadilika.

“Acha nikutengeneze. Najua ninaweza
kukufanya ukawa juu kuliko unavyowaza. Unacho kipaji kikubwa sana Laura.”
Chris alikuwa akizungumza kwa hisia kali sana. Hata hivyo si kweli kwamba, Laura alikuwa na kipaji cha kuigiza – alikuwa mrembo! Hiyo ilikuwa gia tu ya kumwingiza kwenye kumi na nane zake.
Laura aliachia tabasamu pana. Moyoni Chris akaugulia maumivu ya shoti ya mapenzi. Alizidi kuchanganyikiwa. Kila dakika, kila sekunde, uzuri wa Laura uliongezeka.

Pamoja na kuelezwa yote hayo, Laura
hakuzungumza chochote. Alibaki kimya tu akimwangalia Chris. Macho yao kuna
wakati yaligongana na wote hawakuweza kuhimili kuangaliana japo kwa sekunde
tano tu mfululizo.
Tayari kuna kitu kilianza kuingia moyoni mwa Laura lakini hakukiamini sana. Eti ameanza kumpenda Chris!
“Siyo kweli. Hizi si hisia zangu. Ni pombe tu,” akawaza.

Ghafla Chris akasimama. Alifanya
kitendo hicho kwa haraka sana kama aliyeamrishwa. Alirudi nyuma kidogo hadi
alipofikia kitandani. Akachukua taulo kubwa pale kitandani kisha akalitupa
begani mwake.
“Samahani...” akasema Chris.
“Ndiyo!”
“Naingia bafuni kidogo.”
“Samahani...” akasema Chris.
“Ndiyo!”
“Naingia bafuni kidogo.”
“Sawa.”
Chris akapiga hatua nyingine fupi, akaufikia mlango wa kuingia bafuni. Akashika kitasa na kukinyonga kidogo. Mlango ukafunguka. Mara moja akaingia, halafu akaufunga.
Punde tu maji yalianza kusikika yakichuruzika. Chris alikuwa anaoga. Alipomaliza, alijikausha vizuri kisha akajifunga taulo yake kiunoni. Akabeba zile nguo zake na kutoka mle bafuni.

Kwa Laura lilikuwa tukio la ajabu
sana. Chris aliingia chumbani na taulo tu. Ajabu kubwa ni Chris kutoka na taulo
lakini lingine ni mshangao wa mwili wa Chris.
Kutoka moyoni, Laura alikiri kuvutiwa na mwonekano wa Chris. Taulo lilimfanya mwili wake uonekane kwa ukamilifu wake. Kifua cha mazoezi kilionekana dhahiri, huku tumbo lake likiwa limefunikwa na bustani nzuri ya kupendeza!

Siku zote Laura amekuwa
akichanganywa zaidi na miili ya wanaume wa namna hiyo. Shoti ya umeme wa
mapenzi ikahamia kwa Laura. Bado alikiri kuwa hajampenda Chris lakini angalau
kwa usiku ule angemfaa sana!
“Oooooh! Kumbe yupo hivi? Hebu angalia jamani. Chris ananipa mateso sasa,” akawaza Laura alipomwangalia Chris tumbo lake.

“Samahani kwa mara nyingine,
sikujali kutoka na taulo kwa sababu najua hakuna tatizo. Wewe ni rafiki yangu.
Au nimekosea?” Chris akasema.
“Uko sawa.”
Chris akafungua begi lake kisha akatoa bukta na tisheti, akarudi tena bafuni. Huko alivaa kisha akarudi tena chumbani. Mawazo yalimjaa Chris. Ni kweli alimtaka sana yule mrembo usiku ule lakini aliogopa angeweza kumkosa kama angemwambia mambo ya mapenzi mapema.

Wazo lake kichwani alijua amepata
mke, siyo demu wa kuzugia! Mwisho aliamua kuzishinda hisia zake ili aweze
kutengeneza kitu chenye manufaa mengine makubwa zaidi mbele yake.
Angejua!!!
Angejua!!!
Laura yeye aliumizwa sana na mwili
wa Chris. Alitamani sana asikie akimwambia angehitaji kuwa naye usiku ule. Ni
kwa usiku ule tu! Laura hakuwa na chembe ya mapenzi ya kudumu na Chris.
Hakuna aliyejua kilichokuwa moyoni mwa mwenzake.

Itaendelea Kesho.
Post a Comment