Kampuni yajitokeza kudhamini picha ya mtoto wa Diamond
INAWEZEKANA
baada ya siku chache mashabiki wenye kiu ya kuona sura ya mtoto wa mwanamuziki,
Nasibu Abdul ‘Diamond’, Latifah, ikakatika baada ya msanii huyo na mzazi
mwenzake, Zarinah Hassan, kuweka wazi siku maalum watakayomuonyesha mtoto huyo
hadharani.
Tangu
mtoto huyo azaliwe takribani siku 30 zilizopita, sura yake imekuwa ikifichwa
lakini juzi usiku wazazi wake walitoa tamko kupitia kurasa zao za Mtandao wa
Kijamii wa Instagram kuwa Septemba 20, mwaka huu rasmi wataonyesha sura ya
mtoto huyo baada ya mdhamini kujitokeza kudhamini zoezi hilo.
“Tarehe
20/9/2015, kwa mara ya kwanza sura ya binti yangu @princess_tiffah tutaiweka
hadharani… Je ungependa kujua ni kampuni gani imedhamini video na picha yake ya
kwanza? Usikae mbali na mimi… inakaribia,” yalikuwa ni sehemu ya maneno
aliyoandika msanii huyo kabla ya muda mfupi ujumbe huo pia kuwekwa tena kwenye
‘akaunti’ ya Zari.
Kama
kawaida, baada ya hayo, kuliibuka ‘comments’ nyingi juu ya ujumbe huo kutoka
kwa mashabiki ambapo wapo walioponda kuhusiana na hilo lakini watetezi na
waliojibu mashambulizi hayo pia walichukua nafasi yao na kumpongeza msanii
huyo.

Post a Comment