IKIWA UCHAGUZI MKUU UTAFANYIKA LEO, LOWASSA ATASHINDA KWA 52.1%
Zikiwa zimesalia siku 47 kabla ya kufika October 25, utakapofanyika uchaguzi mkuu nchini, Asasi ya kiraia ya "Elite Generation" imefanikiwa kuainisha Takwimu za makadirio ya wapiga kura mwaka huu na namna wagombea wa Urais wanavyokubalika.
Ripoti ya utafiti huo inaonesha kuwa ikiwa uchaguzi utafanyika leo mgombea wa CHADEMA anayeungwa mkono na vyama vinavyounda UKAWA Mhe.Edward Lowassa atashinda kwa 52.1% ya kura zote, akifuatiwa na mgombea wa CCM anayetegemewa kupata 32.6% ya kura zote zitakazopigwa. Wagombea wengine kwa pamoja watapa chini ya 20%.
Kwa mujibu wa Tume ta Taifa ya Takwimu, Makadirio ya Idadi ya Wapiga Kura Mwaka 2015 ni watu 24,253,541. Tanzania Bara wapiga kura ni watu 23,533,050 na Zanzibar wapiga kura ni 720,491.
Mkoa wenye wapiga kura wengi ni Dar es Salaa ambao una wapiga kura 2,932,930 na mkoa wenye wapiga kura wachache zaidi ni Kusini Unguja yenye wapiga kura 69,546.
Hali inaonesha kuwa kati ya mikoa 25 ya Tanzania Bara, UKAWA inaungwa mkono zaidi katika mikoa 11 na CCM mikoa 8, huku mikoa 6 UKAWA, CCM na vyama vingine wakigawana wafuasi na kuzidiana nguvu katika majimbo ya mikoa hiyo.
Kwa upande wa Zanzibar, UKAWA inaungwa mkono mikoa miwili, CCM mikoa miwili na mkoa mmoja wakitoshana nguvu.
TANZANIA BARA,
Mikoa ambayo UKAWA ina wafuasi wengi kwa Tanzania Bara ni Dar es Salaam yenye wapiga kura (2,932,930), Arusha (944,729), K'njaro (976,003), Tanga (1,120,310), Morogoro (1,264,829), Mwanza (1,403,743), Mara (834,580), Mbeya (1,477,365), Iringa (524,390), Shinyanga (762,317), na Manyara (744,571).
Kwa upande wa CCM inaungwa mkono zaidi mikoa ya Dodoma (1,095,318), Pwani (644,840), Lindi (518,230), Ruvuma (783,296), Katavi (271,160), Mtwara (773,289), Singida (698,910), na Rukwa (472,796).
Mikoa ambayo UKAWA, CCM, ACT na vyama vingine vinatoshana nguvu hadi sasa ni Kagera (1,217,388), Kigoma (1,032,161), Tabora (1,124,167), Geita (808,337) Njombe (392,634) na Simiyu (714,757).
MIKOA YA Z'BAR
CCM inaungwa mkono zaidi Kaskazini Unguja yenye wapiga kura 104,965 na Kusini Unguja yenye wapiga kura 69,546.
UKAWA inakubalika zaidi mikoa ya Kaskazini Pemba yenye wapiga kura 103,910 na Kusini Pemba yenye wapiga kura 95,546. Mkoa wa Mjini Magharibi wenye wapiga kura 346,524 UKAWA na CCM wanakadiriwa kuwa na wafuasi wanaolingana.
UCHANGANUZI.
Katika mikoa 13 ambayo UKAWA inaungwa mkono (11 bara na 2 Zbar), mikoa hiyo ina juma ya wapiga kura 13,185,223. Ikiwa asilimia 70% ya watu wa maeneo hayo wakiipigia UKAWA basi mgombea wa UKAWA atapata kura 9,229,656, Mgombea wa CCM atapata kura 2,737,680 na wagombea wa vyama vingine watapata kura 1,217,887.
Katika mikoa 10 ambayo CCM inaungwa mkono (8 Bara na 2 Zbar) mikoa hiyo ina jumla ya wapiga kura 5,432,350. Ikiwa asilimia 70% wataipigia CCM basi mgombea wa CCM atapata kura 3,802,646, mgombea wa UKAWA atapata kura 1,073,686 na wagombea wa vyama vingine watapata kura 556,018.
Katika mikoa 7 ambayo UKAWA, CCM na vyama vingine vinashindana, mikoa hiyo ina jumla ya wapiga kura 5,635,968. Ikiwa vyama hivi vitaendelea kulingana nguvu basi kila kimoja kinaweza kupata kura zisizozidi 1,859,869.
MAJUMUISHO.!
Kutokana na takwimu hizo hapo juu, ikiwa uchaguzi mkuu utafanyika leo;
1. Wagombea wa vyama vingine (ACT, CHAUSTA, DP, TLP etc) kwa pamoja watapata kura 4,070,160 sawa na asilimia 14.9% ya kura zote.
2. Mgombea wa CCM atapata kura 8,400,195 sawa na 32.6% ya kura zote.
3. Mgombea wa UKAWA atapata jumla ya kura 12,163,228 sawa na asilimia 52.1% ya kura zote.
4. Jumla ya kura 72,760 sawa na asilimia 0.3% ya kura zote zinategemewa kuharibika.
Kazi hii ilifanyika Dodoma this weekend. Thanks Dodoma. See u next time.!

Post a Comment