Wema aibu mpyaa! Anaswa na mwanaume wakifanya yao hotelini!
Mwandishi wetu
Licha
ya kudai kwamba skendo za ngono sasa basi, staa wa sinema za Kibongo,
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amekwaa aibu mpya baada ya picha zake kunaswa
akiwa na mwanaume mwingine kwa mara nyingine, mwenye asili ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakiwa kwenye Mgahawa wa hoteli iliyotajwa
kwa jina la Cape-town Fish Market iliyopo Msasani jijini Dar.
MADAI MAZITO
Chanzo
chetu ambacho ni makini kilipenyeza kuwa, katika tukio hilo la hivi
karibuni, staa huyo alikuwa hafahamiani na mwanaume huyo, lakini kuna
kijana mmoja ambaye mara nyingi anawakuwadia mastaa wa Bongo kwa
matajiri, alidaiwa kumtonya Wema kuwa kuna ‘mchati’ anataka kutoka naye.
Kilifunguka
kwamba, baada ya Wema kung’atwa sikio juu ya Mkongomani ambaye ana
‘hela chafu’, alidaiwa kuonekana kuchachawa hivyo eti alikubali
kupelekwa kwake akajazwe ‘mihela’.
WAKUTANA, WAFANYA YAO
Chanzo
hicho kilizidi kumwaga habari za jikoni kuwa baada ya Wema kufika
hotelini hapo, alitambulishwa kwa Mkongo huyo ambapo baada ya
kusalimiana tu, walikaa pamoja na kuanza ‘kufanya yao’.
WAJIACHIA PICHA WAAA!
Mpashaji
wetu alizidi kufunguka kuwa baada ya kukaa na kupata kinywaji cha
kutosha, walianza kupiga picha mbalimbali bila kujali kama kuna watu
wanaweza kuwapiga picha na baada ya hapo walianza kupigana mabusu
yaliyowaacha hoi wapiga chabo a.k.a wavimba macho.
“Yaani
baada ya pombe kukolea, ilikuwa ni balaa. Wema wala hakuona aibu tena,
walikuwa wakipiga picha mbalimbali mpaka wanapigana makisi ya mdomoni
kitu ambacho watu wengi walikuwa wakikishangaa sana,” kilisema chanzo
hicho.
MKONGO ‘AMB-LOCK’
Mpashaji
huyo alidai kwamba, baada ya Wema na Mkongo huyo kukutana na kumaliza
‘shida’ zao, kila mtu alichukua hamsini zake huku jamaa huyo
‘akim-block’ Wema kwenye simu.
WEMA ANASEMAJE?
Baada ya kujazwa habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Wema kusikia anasemaje, lakini simu yake haikuwa hewani.
Alipofuatwa
nyumbani, habari zilizopatikana zilieleza kwamba, Wema alikuwa Dodoma
kwenye vikao vya uteuzi wa wagombea Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM).
Baada ya taarifa hizo, gazeti hili lilitimba kwenye hoteli hiyo kumsaka Mkongo huyo lakini lilielezwa kuwa ameshatimua.
NI AIBU MPYA?
Ukimwacha
Mkongo huyo, huko nyuma Wema aliwahi kuripotiwa kutoka na wanaume
kadhaa wakiwemo, TID, Mr Blue, marehemu Steven Kanumba, Yusuf Jumbe
Yusuf, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na
CK huku wengine zikiwa ni skendo tu na mwenyewe kuzikanusha.


Post a Comment