ad

ad

MGEJA, GUNINITA WAKITOSA CHAMA CHA MAPINDUZI, WAJIUNGA CHADEMA

Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam, Sheikh, Rajab Katimba (kushoto) akiwa na  aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga ambaye ameachana na chama hicho, Khamis Mgeja,  na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita, ambaye naye amehamia Chadema. 2.Mgeja akionesha ishara ya Chama Cha Demokrosia na Maendeleo mara tu baada ya kutoa tamko.
Mgeja akionyesha ishara ya Chadema baada ya kutoa tamko la kujiuzulu. 3.Wanahabari wakichukua tukio.
Wanahabari wakichukua matukio katika hafla hiyo. 4.Baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi alioungana nao kuelekea chama Cha Chadema.
Baadhi ya makada wa CCM alioungana nao kujiunga na Chadema.
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita, wametangaza  kuachana na chama hicho na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Mwenyekiti huyo alitoa kauli hiyo leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) alipokuwa akiongea na wanahabari jijini Dar es Salaam, ambapo alisema kuwa umamuzi wa kuachana na CCM ulitokana na kutoridhika na uteuzi wa mgombea kupitia chama chake,  John Pombe Magufuli,  pamoja na mwenendo mzima wa chama hicho kwa viongozi kufanya wanachokitaka wao.
Amesema kuwa  uteuzi wa mgombea urais uliofanyika Dodoma chini ya mwenyekiti wa chama hicho,  Jakaya Mrisho Kikwete, haukuzingatia taratibu na maadili ya chama ambapo alisema ulijaa upendeleo na  chuki dhidi ya aliyekuwa akimtegemea, yaani waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Ngoyayi Lowassa.
Aidha Mgeja alisema amekuwa ndani ya CCM zaidi ya miaka 20 na haoni haja ya kuendelea nacho kwani hakijaonesha mapenzi mema kwa mgombea aliyekuwa akikubalika kwa wananchi.
Katika maelezo yake Mgeja alitumia kauli ya hayati  Julius Nyerere,  aliyotoa mwaka 1995 kwamba:  “Watanzania wanahitaji mabadiliko na wasipoyapata ndani ya (CCM) watayatafuta nje ya CCM.”
NA DENIS MTIMA/GPL
Powered by Blogger.