JAMANI DADA MARTHA LOOO!-21

www.facebook.com/2jiachie
ILIPOISHIA
“Dogo hujambo?” alimsalimia muuzaji.
“Sijambo.”
“Eti, huyu kaka anayekaa hapa huwa anafika muda gani?”
SASA ENDELEA...
“Mh! We ni nani kwani?”
“Mgeni wake.”
“Kutoka wapi?”
“Tanga.”
Muuza duka huyo alimkodolea macho Martha akiwa anaonekana haamini kama alitokea Tanga. Tanga bila hata kibegi cha nguo!!
“Kwani namba yake ya simu huna?” aliuliza muuza duka huyo.
“Nampigia hapokei. Nikasema nije hadi hapa ili kama anakuja muda huu nimsubiri kama si muda wake nikatafute gesti ya kulala.
Muuza duka huyo alijua kuna kitu kilimfanya Roi asipokee simu. Na kitu hicho si kingine ni jamaa huyo kuzama ndani na mwanamke mwingine aliyekuwa amekaa kwenye benchi nje ya duka lake.
Kwa hiyo uamuzi ulikuwa kwake. Aseme ukweli au adanganye.
Moyoni mwake aliona Roi mwenyewe alitakiwa kuwa muwazi katika mipango yake kuhusu wanawake. Si vizuri kugonganisha...
‘’Mimi nimemwona kaingia ndani muda si mrefu,’ alisema muuzaji huyo.
Martha akashangaa...
“Kwa miguu?” aliuliza.
“Na gari.”
Martha alitupia macho kwenye geti na kubaini kwamba, ni kweli gari linaweza kuwemo ndani halafu mtu aliye nje asilione...
“Aliingia na nani?”
“Mwanamke mmoja hivi. Alimsubiri kwa muda mrefu hapohapo nje.”
“Mwanamke mmoja hivi! Kavaaje?”
“Huyo mwanamke kavaa haya magauni yenu ya siku hizi, marefu mpaka miguuni, amelaza nywele kwa nyuma, mweupe kiasi, ana figa namba nane.”
Kwa haraka sana, Martha alimuweka kichwani mama Anna kwani anakumbuka ndiye aliyevaa hivyo inavyosemwa.
“Huyo ni mama Anna tu. Yaani kumbe...mh! Yaani mama Anna na Roi ni wapenzi? Mbona siamini. Wameanzaje kwanza?”
Martha aliinua simu yake akampigia mpangaji mmoja na kuzungumza naye...
“Hivi unaweza kuamini mama Anna alipotoka hapo kumbe amekuja nyumbani kwa yule mtu wangu?”
“Kweli?”
“Kabisa. Nimepewa ushahidi wote.”
“Kwa hiyo?”
“Wamo ndani na geti limefungwa.”
“Mh! Mama Anna naye bwana. Ana maana gani sasa kufanya hivyo kwa mtu wa karibu kama wewe?”
“Ndiyo hapo sasa. Mimi leo sitoki hapa getini. Nipo tayari hata kulala hapahapa,” alisema kwa uchungu Martha na kukata simu.
***
Roi na mama Anna walikuwa chumbani sasa, kitandani, wakigalagazana kwa mahaba mazito huku mwanamke huyo akilia kilio cha uongo ili kumkoleza zaidi mwanaume huyo pale kitandani.
Wote walikuwa wamelegea macho kwani kwa mama Anna yeye alishajua jinsi ya kumnasa Roi huku yeye Roi akiwa hoi bin taaban.
Simu ya mama Anna iliita mpaka ikakata, ikaita tena mpaka ikakata, ikaita tena...
“Mh! Hiyo simu itakuwa ya umuhimu kwangu,” alisema Roi na kumtaka mama Anna aipokee...
“Hakuna lolote, haina umuhimu wowote, ngoja niizime tu,” alisema mama Anna akiifuata.
Kabla hajaizima aliangalia missed calls akakuta mbili na zote ni za wapangaji wenzake, akahisi kitu. Akampigia wa kwanza...
“Vipi mama nanihii...”
“Mwenzangu, Martha yupo getini. Kasema ana ushahidi umo ndani kwa jamaa yake na hatoki mpaka kesho asubuhi.”
Palepale mama Anna alikata simu, akamwangalia Roi. Naye Roi akamuuliza...
“Vipi kwani?”
“Martha yupo getini. Lakini ishu si hiyo bali amejua mimi nimo ndani, eti ana ushahidi.”
Roi alikumbuka kwamba, atakuwa ameambiwa na muuza duka ambaye alishuhudia kila kitu...
“Mmh! Atakuwa ameambiwa na muuza duka. Loo! Sasa?”
“Hata sijui. Kwani wewe hofu yako ipo kwa kiasi gani?” mama Anna alimuuliza Roi.
“Mimi sina wasiwasi wowote ule. Nimeamua kuwa na wewe japo kibinadamu nitakuwa nimefanya makosa makubwa, kumuumiza mtu jambo ambalo silipendi katika maisha yangu,” alisema Roi kwa sauti ya upole.
Alitoka kitandani, akavaa. Mama Anna naye akatoka kitandani, akamfuata kwa nyuma yeye akiwa amejizungusha upande wa kanga. Walifika sebuleni, wakaangalia kwa nje kupitia nafasi ya matundu ya ukuta wa fensi. Walimwona Martha amesimama dukani akizungumza na muuza duka.
Sura ya Martha ilitafsiri uchungu wa maumivu ya kutendwa. Ikawa kama imejikunja, Roi akahisi huruma...
“Martha... Wajina wako anaumia sana. Sasa itabidi nikutoe kiaina. Pita mlango wa nyuma, nenda mahali hapo nyuma kuna baa, kakae.”
“Mh!” Aliguna mama Anna, akatoa wazo...
“Sawa lakini turudi chumbani, nipe haki yangu kwanza ndiyo nitoke, siwezi kutoka hivihivi wakati uliishaanza kunipandisha mzuka wangu na mzuka wangu ukinipanda mimi akili zinachanganyikiwa kabisa.”
“Kuhusu hilo tu, twende sasa hivi.”
Walikwenda chumbani ambako Roi aliikuta simu yake ikiendelea kuita kwa namba ya Martha.
Mama Anna alikimbilia moja kwa moja kwenye kitanda huku akitupa kanga chini.
Alipokuwa juu ya kitanda akakaa mkao wa mechi tayari akijua anatakiwa kutoka ndani ya nyumba hiyo lakini moyoni alihakikisha anatoa mapigo ambayo, Roi anaweza kuamua asitoke tena na Martha kama kulala nje ya geti alale tu.
Roi, kuona mkao wa mama Anna alichanganyikiwa. Kama paka aliyeona panya. Akaenda kitandani kwa staili ya kuruka kama golikipa wa timu maarufu ya Ulaya...puu!!
Je, nini kilitokea? Usikose kwenye Gazeti la Risasi Mchanganyiko, Jumatano ijayo.
Post a Comment