AZIZA WA FACEBOOK - 4

ILIPOISHIA:
MIMI: Hilo usijali.
Katika kipindi hicho nilikuwa nafikiria mambo mengi sana, huyu mtoto kwangu alionekana kuwa na pozi ajabu, yaani nilikuwa nikizipitia post za kizushi alizokuwa akiziweka, watu walikuwa wakicomment halafu yeye hatokei.
SASA ENDELEA:
Hata kama kaweka picha ya mdoli, watu walikuwa wakicomment halafu yeye hatokei na mbaya zaidi kulikuwa na watu wengi wanaolike na kucomment jambo lililonifanya kugundua kwamba kuna siku huyu msichana alikwishawahi kuweka picha na hivyo wanaume kujua ni mzuri kisha kuzitoa.
Bado kiu yangu ilikuwa ni kuwasiliana na Aziza tu ambaye alionekana kuwa mtu wa mapozi sana. Sikujua ningeanzia wapi ila nilichokifanya ni kuanza kumtumia meseji nione kama angeijibu au kuipotezea.
MIMI: Mambo!
Niliituma meseji hiyo, siku ya kwanza, ya pili, ya tatu mpaka wiki hadi mwezi lakini meseji ile moja haikujibiwa, mbaya zaidi nilikuwa namuona yupo hewani. Sikukoma kidume mimi, bado nilikuwa nikimtumia meseji za kumsalimia lakini hali ilikuwa ileile, hakujibu.
Mtu mzima nikaona naumbuka, kama nilikuwa naitwa Sharukh Khan basi ilibidi niwaonyeshe watu kwamba hawakukosea kuniita jina hilo, nilitaka kuwaonyeshea dhahiri kwamba mama yangu alikuwa mtu wa Tanga, kule ambapo mapenzi yalikuwa yamenogeshwa kwa kuwekewa makorokocho. Nilichoanza kukifanya ni kuanza kumtag picha. Hapa ni lazima ugundue, picha ambazo nilikuwa nikimtag ni zile ambazo zilikuwa na muonekano wa kimapenzi tu. Picha ambazo zilikuwa zikiwaonyesha wapenzi wakibusiana na kukumbatiana, ndizo ambazo nilikuwa nikimtag, tena yeye peke yake.
Hahaha! Ule ukaonekana kama ujinga vile kumbe kwa wakati huo nilikuwa na target zangu kichwani. Niliendelea na mtindo ule mpaka siku ambayo akaonekana kuchoka na kukasirika, kwa mara ya kwanza akaja inbox, ila siyo kiamani kama nilivyotaka, alikuja kibifu.
AZIZA: Naomba usiwe unanitag mapicha yako.
Niliisoma meseji ile. Kwanza nikacheka, kilichonifanya kucheka ni kwa kumuona kwamba alikuwa msichana mjinga sana, kitendo cha yeye kuniandikia meseji kilionekana kuwa kama kosa kubwa sana, nilichokifanya, nikaanza kuandika meseji ndefu, meseji ambayo ingemfanya kunijibu, meseji ambayo isingemfanya kubaki kimya.
MIMI: Kuna vitu kadhaa Aziza itakupasa uelewe na ninatumaini vitakuongoza katika maisha yako yote. Jitahidi kuishi lakini kamwe usiwe mbinafsi. Unapopata kitu, usitake kukaa nacho, jaribu kuchangia pamoja na wenzako. Unapopata chakula, jaribu kumwangalia yule asiye na chakula na kumgawia, milele atakushukuru kwa ulichomfanyia siku moja tu alipokuwa na njaa.
Unapomuona mtu hana nguo, mgawie nguo na ataendelea kukushukuru maisha yake yote. Unaniona mimi, mimi si mbinafsi hata mara moja, katika maisha yangu nimekuwa nikiwapa watu vitu fulani vitu ambavyo hawana katika maisha yao, nikakuangalia wewe, nikakuona kwamba u maskini sana, ukijiangalia, unajiona kuwa tajiri, mwenye fedha labda, lakini bado ni maskini, maskini wa kitu kimoja ambacho ulihitaji mtu mwenye kitu hicho akusaidie, nikakusaidia lakini unaonekana kuukataa msaada wangu. Kuwa makini Aziza, mara nyingine msaada huja mara moja na kupotea, unapoutafuta, inawezekana usiuone tena.
Kwanza nikashusha pumzi nzito, nikaiangalia meseji ile na kisha kuirudia rudia mara nyingi kisha kuituma. Niliiona kuwa meseji kali ambayo isingemfanya kubaki kimya kwa kutaka kujua ni kitu gani ambacho alikuwa amekosa katika maisha yake, kilichonifurahisha, akatuma meseji. Kuna nini tena? Meseji ya pili hiyo, hakujua kwamba ndiyo mwanzo wa chating yetu.
AZIZA: Umemaanisha nini?
MIMI: Nimemaanisha kwamba wewe ni maskini. Tena yule fukara kabisa. Hiyo ndiyo maana yangu.
AZIZA: Sijakuelewa.
MIMI: Hebu isome vizuri hiyo meseji, utaielewa tu.
AZIZA: Nimeirudia zaidi ya mara tano, sijaielewa, naomba uniambie umemaanisha nini?
MIMI: Nikuulize kitu kimoja?
AZIZA: Niulize.
MIMI: Unaweza kugundua ni umaskini wa aina gani umekuwa nao?
AZIZA: Hapana na ndiyo maana nikauliza.
MIMI: Inawezekana ukawa na magari, nyumba na fedha ila bado ukawa maskini, unakubaliana nami?
AZIZA: Hapana.
MIMI: Kwa sababu gani?
AZIZA: Mtu ana kila kitu, atakuwaje maskini.
MIMI: Hahahah! Aziza. Ukisema hivyo unakosea. Kuwa na kila kitu haimaanishi kwamba wewe si maskini. Unaniruhusu nikuulize kitu?
AZIZA: Niulize
MIMI: Unaamini katika fedha?
AZIZA: Yeah!
MIMI: Fedha inaweza kukupa kila ukitakacho?
AZIZA: Yeah!
MIMI: Unakosea sana Aziza.
AZIZA: Unapokuwa na fedha unanunua gari ulitakalo, unanunua chakula, unanunua nyumba na mambo mengine. Kwani nimekosea?
MIMI: Umepatia. Ila unavyoona kila mtu mwenye fedha huwa na furaha?
AZIZA: Inawezekana.
Itaendelea siku ya keshoooooo
Post a Comment