ROBIN VAN PERSIE NDO BASI TENA MANCHESTER UNITED
Baada ya kucheza England kwa miaka 11, mshambuliaji nyota wa Manchester United, Robin van Persie anaachana na Premier League na kwenda kujiunga na Fenerbahce ya Uturuki.
Mwenyekiti wa Fenerbahce Aziz Yildirim amethibitisha kuwa mazungumzo ya uhamisho yamekamilika na Van Perise anatarajiwa kutambulishwa rasmi Jumatatu kufuatia uhamisho wa ada inayokaridiwa kufikiwa pauni milioni 3.4.
"Tumefanya kazi kubwa hadi usiku wa manane. Tukapokea fax tano na sisi tukatuma sita na hatimaye tukafikia muafaka (na Manchester United)," ananukuliwa Yildirim.
Kwa upande wake, Van Persie, Jumamosi alionekana akiagana na rafiki yake wa karibu Alderley Edge mmiliki wa mgahawa jijini Manchester.
Robin van Persie anakwenda kujiunga na Fenerbahce
Van Persie akisema kwaheri kwa swahiba wake Alderley Edge
Van Persie anakwenda kucheza nje ya England kwa mara ya kwanza baada ya miaka 11 ya kuitumikia Premier League
Van Persie akiagana na rafiki yake wa miaka mitatu katika jiji la Manchester
CREDIT: SALUTI 5.COM

Post a Comment