MANCHESTER CITY YASHINDA VITA YA RAHEEM STERLING
Manchester City sasa imepewa idhini na Liverpool ya kumsajili winga Raheem Sterling baada ya dau lao la pauni milioni 49 kukubaliwa. WACHEZAJI GHALI ZAIDI PREMIER LEAGUE 1. Angel di Maria (Man United) £60m 2. Fernando Torres (Liverpool) £50m 3. Mesut Ozil (Arsenal) £42.5m 4. Sergio Aguero (Man City) £38m 5. Juan Mata (Man United) £37m 6. Andy Carroll (Liverpool) £35m 7. Alexis Sanchez (Arsenal) £35m 8. Fernandino (Man City) £34m 9. Robinho (Man City) £32.5m 10. Eliaquim Mangala (Man City) £32m Kwa mujibu wa magazeti mbali mbali ya mitandaoni ya Uingereza, Manchester City italipa pauni milioni 45 lakini pia kutakuwa na pauni milioni 4 ambazo zitaongezwa kutegemea na maendeleo ya mchezaji huyo ndani ya Etihad. Sterling sasa anatarajiwa kumalizana na City katika upande wa maslahi binafsi kabla ya kwenda kufanya vipimo vya afya na hatimaye kukamilisha usajili wake wa bei mbaya. Kwa mujibu wa rekodi za usajili, Sterling atakuwa mchezaji ghali wa tatu kwenye Premier League akiwa nyumba ya Angel Di Maria na Fernando Torres. Mara atakapokamilisha usajili wake, Sterling ambaye mkataba wake Liverpool ungemalizika mwaka 2017, atakuwa ndiye mchezaji ghali zaidi miongoni mwa wanasoka raia wa England.

Post a Comment