| Waziri
wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb.)
akifungua Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki
ambao pamoja na mambo mengine utapokea na kujadili taarifa ya ziara ya
Mawaziri nchini Burundi kuhusu hali ya kisisasa nchini humo. Mkutano huo
ambao ni maandalizi ya Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi
utakaofanyika tarehe 06 Julai, 2015, umefanyika kwenye Hoteli ya Serena,
Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Julai, 2015. |
Post a Comment