JAMANI DADA MARTHA LOOO!-11

ILIPOISHIA
Wiki moja ilikatika tangu mazishi ya mume wa shangazi yake Martha, siku hiyo Martha alikaa kwenye mgahawa mmoja akimshukuru Roi kwa ushirikiano wake katika msiba...
“Wala usijali dada yangu. tuko pamoja.”
“Yaani bro kusema ukweli umenipa kampani kubwa sana.”
“Usijali dada yangu.”
“Asante sana,” alisema Martha huku akimwangalia Roi, wakakutana macho, wote wakajikuta wakisisimka...
“Brooo,” aliita Martha kwa sauti iliyojaa mahaba.
SHUKA NAYO SASA...
“Yes sista...”
“Uko sawa?”
“Yeah! Nipo sawa sista, wewe je?”
“Mh!” aliguna Martha bila kusema kama yuko sawa au la!
“Mbona umeguna sista?”
“Mh! We acha tu.”
“Nini?”
“Nimekumbuka mbali.”
“Mbali wapi sista? Umemkumbuka marehemu tuliyemzika hivi karibuni?”
“Wala! Yule ameshapita, nitaendelea kumkumbuka kibinadamu tu lakini si kwa sababu ya hivi ninavyowaza,” alisema Martha.
Roi ilibidi awe mpole tu sasa kwani hakujua nini kiliendelea ndani ya nafsi ya Martha. Walishakubaliana kwamba wabaki kuwa kaka na dada kwa hiyo aliamini ukaka na udada upo vilevile.
Martha alinyoosha mkono na kushika vidole vya mikono ya Roi na kuviminyaminya kiaina huku akimwangalia kwa macho yaliyojaa hamasa ya mahaba...
“Kaka...”aliita kwa sauti ya chini sana, kama vile mgonjwa...
“Niambie dada ‘angu mpenzi!”
“Nakupenda kaka ‘angu mzuri. Umenisaidia sana.”
“Wala usijali sista.”
“Endelea kunisaidia na kunijali hivyohivyo my bro,” alisema Martha huku akiendelea kuvisuguasugua vidole.
Kwa mbali, Roi alishajua kuwa Martha alikuwa hoi kimapenzi, alihitaji mwanaume lakini sasa akawa anajiuliza watakuwa wakiendelea kusuasua mpaka lini? Mara kaka na dada, mara wapenzi...
“Mimi nitakusaidia mpaka mwisho wa ukaka na udada wetu.”
Martha alilegeza macho, akajipeleka na kumwegemea Roi begani huku akirembua...
“Darling...” aliita Martha...
“Yes sweet.”
“Mmh!” aliguna Roi.
“Nini tena?”
“Najisikia uvivuuvivu...”
“Umechoka?”
“Wala sijachoka.”
“Uvivu wa nini sasa?”
“Hata sijui, kama napenda kulala vile...”
“Kwa hiyo una usingizi?”
“Wala.”
“Sasa nini jamani sista?”
“Ah! Mi sijui bwana,” alisema Martha huku akipeleka mkono wake wa kulia hadi kwenye sehemu ya mbele ya suruali ya Roi...
“Da! Sista...”
“Abee...”
“Umefikia huko?”
“Ah! Mimi sijui bwana...sielewi kwa nini nashindwa kushika ahadi wakati naiweka mwenyewe... lakini hata hivyo leo tukienda tusifanye lolote, tukakae tu, tuzungumze halafu baadaye tuondoke. Kama tutazidiwa, labda tufanye romansi tu,” alisema Martha akijaribu kuweka mwongozo wake...”
“Kwa hiyo?” aliuliza Roi kwani sasa na yeye moyoni alisema liwalo na liwe, akawaza...
“Kwanza ni kweli si ndugu yangu, hanihusu kwa lolote lile, sasa nahangaika naye wa nini?” alisema moyoni Roi, akamshika mgongoni Martha, Martha akasisimka kwa kusema maneno yenye kuashiria kusisimka...
“Wewe tu...”
“Basi twende.”
“Wapi?”
“Popote pale penye utulivu.”
“Kwani hapa si hotelini! Kwa hiyo pana vyumba.”
“Nadhani.”
Roi alisimama, akaingia ndani na kutoka baada ya dakika mbili tu, akasimama na kumwita Martha kwa ishara ya mikono, wakaenda vyumbani.
Walichukua chumba kimoja, wakazama humo...
“Sista tutaweza kukaa tu na kuzungumza kweli?” aliuliza Roi...
“Tujitahidi kaka, tukiweza leo basi, shetani atakuwa ameshindwa siku nyingine zote,” alisema Martha akijiamini...
“Haya, tutaona sista.”
Walikaa kitandani, safari hii walikaa sanjari wote wakiangalia mlangoni, miguu yao ikining’inia kwenda chini.
“Kwa hiyo kaka we huwezi kukaa na mimi kama hivi huku tunazungumza?” aliuliza Martha huku akimwangalia Roi, Roi naye akamwangalia Martha kwa macho ya kiume, Martha akalegea, lakini akajikaza...
“Mimi nitaweza bro,” alisema Martha huku akimwangukia mapajani Roi...
“Ka...ka ja...ma...ni...”
Je, unajua nini kiliendelea? Usikose kusoma chombezo hili tamu
Post a Comment