ad

ad

JAMANI DADA MARTHA LOOO!-15

 

“Nakusikiliza dada’angu. Liseme hilo unalotaka kulisema.”
Mama Anna alisogea tena, akanyoosha mikono yake yote na kushika mikono ya Roi…
“Ni hivi…” alikohoa kwanza…
SASA JIACHIE MWENYEWE…
Roi alishtuka kidogo kule kushikwa mikono na mwanamke. Na kama mwanaume alihisi joto la mapenzi likimpanda. Akamtumbulia macho huku akihema kwa mbali…
“Unajua wewe ni mwanaume, tena mzuri na unayevutia, si ndiyo?” alisema mama Anna…
“Pengine wewe ndiyo unaniona hivyo dada.”
“Ni kweli. Hivi, yule Martha kweli ni dada yako kama anavyoendelea kututambulisha kila siku?”
Lilikuwa swali lenye mtego mkubwa kwa Roi. Moyoni aliona nusunusu, akisema siyo hajui nini kingetokea akisema ndiyo pia hakujua nini kingetokea. Akaamua kusema siyo ili kama mama Anna ana jambo la siri anataka kumwambia, amwambie.
“Siyo dada yangu.”
“Ni nani wako?”
Roi aliamini kwa jibu lake kila kitu kiko wazi, lakini kwa vile aliulizwa alijibu…
“Ni mchumba wangu.”
“Ok. Ndiye utakayemuoa?”
“Ndiyo maana yake.”
“Ok. Mnaendana lakini. Hata mimi naunga mkono wewe kumuoa wajina wangu Martha,” alisema mama Anna mpaka Roi akashangaa, moyoni akajiuliza…
“Ina maana hili ndilo alilotaka kuniambia mpaka akawa anakaa vizuri? Siyo hili, huyu ana lake jambo.”
“Kumbe na wewe unaitwa Martha?” aliuliza Roi.
“Ndiyo. Mama Anna, ni kwa sababu ya mtoto wangu tu. Naye yuko kwa baba yake, tulitengana kama mwaka wa nne sasa.”
“Ooh! Sawa.”
Mama Anna akamwangalia Roi kwa macho ya wizi, Roi naye alimwangalia kwa macho ya waziwazi…
“Una lingine dada’angu?”
Mama Anna alimwangalia Roi kwa muda kisha akatoa sauti ya chini sana…
“Lingine mi nakupenda.”
“Oo! Asante sana kwa kunipenda,” alisema Roi huku akimwangalia mama Anna kwa macho ya ujasiri.
Mama Anna alipeleka tena mikono yake kwenye mikono ya Roi na kuishika, akaanza kuiminyaminya kimahaba.
Roi akawa mtu wa kujishtukia tu, ulaini wa mikono ya mama Anna ulimuweka katika wakati mgumu, akahisi akianza kutokwa na kijasho chembamba.
Kwa mtu yeyote aliyewaona alijua wawili hao ni wapenzi kwa jinsi walivyokaa karibu.
“Dada Martha,” aliita Roi.
“Abe.”
“Tubaki kuwa dada na kaka.”
“Ni kweli. Lakini mi nakupenda sana.”
“Ndiyo hivyo, tayari ninaye Martha mwenzako. Akijua je?”
“Atajuaje? Au utamwambia jamaniiii?”
“Hapana! Si unajua dunia haina siri! Hata ukifanyia kitu chumbani, tena ukiwa peke yako, watu watajua tu, sembuse sisi dada!”
“Kwani unataka kuniambia sisi ni utu uzima wetu tunaweza kufanya mambo mpaka yakawa hadharani?” aliuliza mama Anna huku akizidi kuviminyaminya vidole vya Roi. Sasa akawa anakikuna kiganja cha mkono wa kulia, Roi akasisimka…
“Hu…we…zi ku…ju…a,” alisema Roi kwa kukatakata maneno yake.
Roi tayari alishapandisha joto la mwili. Kwa ni kusema ukweli, mama Anna naye alijaliwa. Kila sehemu ya mwili wake ilikuwa ina sifa, sijui wakati wa usichana wake alikuaje kama akiwa mama wa mtoto mmoja tu ndiyo hivyo.
Alijua vyema kuyatumia macho yake. Alipomwangalia mwanaume yalionekana kama ya mtu aliyekuwa akitaka kusinzia ‘flani hivi.
“Hawezi bwana. Mimi nitajitahidi kufanya siri ya hali ya juu. Sitamwambia hata mtu mmoja. We niamini mimi.”
Hivi kweli hawezi kujua? Kila ninapomfikiria, namuona kuwa mwanamke mjanjamjanja, naogopa sana,” alisema Roi, japokuwa naye alikuwa amekwishaanza kuzama katika lindi la tamaa ya mapenzi, lakini akajifanya kukaza.
“Haki ya Mungu hatojua, niamini jamani, kweli hatojua,” alisema mama Anna.
“Mh! Ma…Martha…”
“Abee.”
“Uta…weza?”
“Kufanyaje?”
“Ku…fi…cha si…ri?”
“Mi ni msiri sana usinione hivi,” alisema mama Anna huku akizidi kumkuna kiganjani Roi ambaye sasa damu zilikwenda kwa kasi.
Roi kama mwanaume rijali hakuona sababu ya kulaza damu kwa mwanamke huyo ambaye alijilengesha mwenyewe…
“Afadhali ningemtongoza, sasa mwenyewe tu anajileta halafu nimwachie, nitakuwa si mwanaume,” alisema moyoni huku sasa na yeye akianza kumshikashika mama Anna.
Ilipita kama dakika tatu hakuna aliyekuwa akizungumza zaidi ya kuendelea kushikana kiaina. Kilichosikika ni kuhema kwa mama Anna ambaye sasa alionekana kama tayari amechaji.
Roi alimsimamisha, akamshika mkono na kuondoka naye…
“Tunakwenda wapi sasa?” aliuliza mama Anna.
“Wewe twende tu, wala usiogope,” alisema Roi, tayari akili yake ilikwishahama kabisa, kwa kumwangalia tu, ingekufanya ujue tayari penzi lilimchukua.
Je, unajua walikuwa wakienda wapi? Usikose kusoma chombezo hili tamu.......
Powered by Blogger.