ad

ad

JAMANI DADA MARTHA LOOO!-10







www.facebook.com/2jiachie
ILIPOISHIA:
“Mh! Bro, nimewaza mengi. Mimi nimefikia uamuzi huohuo. Lazima tuendelee kuwa kaka na dada ili uhusiano wetu uendelee kudumu zaidi na zaidi,” alisema Martha...
“Mh! Nikwambie kitu Martha..?”
“Niambie bro...”
SASA ENDELEA...
“Hata mimi sasa nimeamua kuwa kuanzia sasa hivi tuwe ndugu, tena wa damu moja! Mimi ni kaka yako, wewe ni dada yangu.”
“Loo! Jamani napiga vigelegele, umenifurahisha sana kaka yangu,” alisema Martha.
“Hata mimi dada nimefurahi sana. Unajua tulikuwa tunafanya makosa makubwa sana. Watu tumekubaliana kuwa kaka na dada sasa hizi tamaa nyingine za kutoka wapi?” aliuliza Roi...
“Ndiyo hapo sasa bro,” alishadadia Martha.
Baadaye waliagana wakakubaliana kuwasiliana asubuhi inayofuata ili kujuliana hali.
***
Martha alilala kwa amani na furaha. Alihisi ameutua mzigo mkubwa sana. Ilipofika saa kumi na moja alfajiri, Martha alipigiwa simu na shangazi yake kuwa, mumewe huyo shangazi amefariki dunia.
“Ha! Shangazi kweli? Mbona sijajua kama alikuwa anaumwa?” aliuliza Martha akianza kulia.
“Kafa ghafla Martha.”
Martha alikata simu, akatoka kitandani na kutungua nguo za kuvaa ili kwenda kwa shangazi yake.
Lakini wakati anatoka akampigia simu Roi...
“Kaka, mume wa shangazi yangu kafa ghafla jamani...eeee..ooo,” alilia.
“Wapi?”
“Nyumbani kwake Magomeni.”
“We uko wapi sasa sista?”
“Mimi ndiyo nakwenda huko.”
“Uko wapi?”
“Nipo hapa kituoni Kimara.”
“Nakuja hapohapo kituoni sista.”
Roi alikurupuka, akatoka mbio hadi kwenye gari, akaendesha hadi kituoni Kimara. Akamchukua Martha kwenye gari hadi Magomeni msibani.
Nyumba yote ililipuka kwa vilio, majirani walijaa nao wakilia sambamba na familia ya marehemu. Martha alifikia kulia akiwa ameishiwa nguvu.
Ilibidi Roi ajumuike na wanaume wengine waliokaa nje ili kuona hali inakwendaje.
Kulipokucha, Martha ndiyo akamkumbuka Roi kwamba hawakuagana baada ya kuachana...
“Ooo! My God! Bro atakuwa ameondoka bila kujua nini kinaendelea!” alisema moyoni Martha, akampigia simu huku akiwaza...
“Sikumfanyia fea hata kidogo. Mtu akupe lifti hadi msibani halafu unamwacha bila kumshukuru.”
Simu ilipokelewa, Martha akashtuka kusikia kelele...
“Bro, upo wapi?”
“Nipo hapa nje sista.”
“Haa! Nakuja.”
Martha alitoka mbio hata waombolezaji wengine wakamshangaa. Alimkuta Roi amekaa kwa kujikunyata akitetemeka baridi.
“Ooh! Pole baby,” Martha alijikuta akisema hivyo.
Alimsimamisha Roi, akamvutia pembeni...
“Nisamehe sana sweet, nilichanganyikiwa. Sikujua kama upo nje, mawazo yangu umeshaondoka,” alisema Martha.
“Nilishindwa kuondoka sista,” alisema Roi kwa sauti ya upole huku akimpa pole Martha kwa msiba...
“Asante sana baby. Sijajua mazishi itakuaje? Lakini kikao kitakaa baadaye kwenye saa nne asubuhi,” alisema Martha.
Roi aliaga, akaondoka huku Martha akimsindikiza kwa macho yaliyojaa huruma...
“Maskini. Yaani amekubali kuacha usingizi wake kwa sababu ya msiba wangu. Huenda Roi si kaka yangu,” alisema moyoni Martha.
***
Baada tu ya kikao cha familia cha kujadili namna ya mazishi ya mume wa shangazi yake Martha, Roi akapiga simu kama alijua vile...
“Kaka...”
“Ee dada! Vipi kuhusu utaratibu?”
“Tunazika kesho saa kumi jioni, Kinondoni.”
“Ooh! Nakutumia shilingi laki moja na nusu kama mchango wangu.”
“Da! Nitashukuru sana kaka yangu.”
“Poa...poa! halafu kesho nitakuja kwenye mazishi.”
“Sawa kaka, sawa.”
***
Ulikuwa mchana wenye mawazo kwa Martha...akiwa ametulia tuli huku wachache wakiendelea kulia, aliwaza...
“Hivi kweli yule ni kaka yangu au mume wangu? Ina maana anaweza kunijali kiasi hiki kweli?” alijiuliza Martha huku akiiangalia meseji ya pesa aliyotumiwa na Roi.
***
Wiki moja ilikatika tangu mazishi ya mume wa shangazi yake Martha, siku hiyo Martha alikaa kwenye mgahawa mmoja akimshukuru Roi kwa ushirikiano wake katika msiba...
“Wala usijali dada yangu. Tuko pamoja.”
“Yaani bro kusema ukweli umenipa kampani kubwa sana.”
“Usijali dada yangu.”
“Asante sana,” alisema Martha huku akimwangalia Roi, wakakutana macho, wote wakajikuta wakisisimka...
“Brooo,” aliita Martha kwa sauti iliyojaa mahaba.
Je, unajua nini kiliendelea? Usikose kusoma chombezo hili tamu sana
Hi! Baada ya kusoma simulizi hii akikisha unashare kuwawezesha marafiki zako kwenda na sisi katika simulizi hii hapa. Share tukutumie sehemu inayofuata mbele.
ITAENDELEA HAPA HAPA USIKOSE
Powered by Blogger.