ad

ad

UZINDUZI WA BONGO STAR SEARCH 2015 “JUKWAA LAKO- KUWA ORIGINAL”

Madam Rita (wa pili kushoto) akizindua awamu nyingine ya shindano la BSS kwa mwaka 2015.
 
Mshindi wa BSS mwaka 2013, Emmanuel Msuya (kushoto) akizungumza jambo na wanahabari (hawapo pichani).

Madam Rita akifafanua jambo wakati wa uzinduzi huo.
 
Kushoto ni Madam Rita, mmoja wa wadau, kulia ni mbunifu wa mitindo nchini Ally Remtullah wakifuatilia uzinduzi huo.
 
Baadhi wa waandishi wa habari wakifuatilia kipindi maalumu cha wasanii na washindi waliopita katika shindano la BSS, miaka ya nyuma.
HATIMAYE kile kipindi cha kuvumbua, kunyanyua vipaji vya wanamuziki kutoka wasipojulikana mpaka kuwa mastaa,
Bongo Star Search “BSS”, kimerudi tena kwa msimu mwingine kikiwa na ubora wa hali ya juuAkizungumza na wanahabari leo wakati wa uzinduzi  huo uliofanyika katika jengo la High Sprit Lounge (IT Plaza) liliyopo Posta jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Benchmark Production, Madam Rita Paulsen alisema “Mwaka 2015 utakuwa ni msimu mzuri na wa kusisimua kwa shindano hili la BSS kwa watazamaji.
Mwaka huu shindano litafanyika kwenye mikoa ya Arusha, Mbeya na Mwanza pia litarushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni vya Star TV na Clouds TV kuanzia Julai, 19 mwaka huu.
 
Sehemu ya waraka kwa Watanzania.

No comments

Powered by Blogger.