JANUARY AMFUNIKA LOWASSA?
NAIBU Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba ambaye
ni mmoja wa makada wa CCM waliotangaza nia ya kuwania kuteuliwa kuwania
Urais, ameibuka na ubunifu wa kisasa katika namna ya kutangaza nia ya
kuwania urais kupitia CCM, kitu ambacho endapo kitafanikiwa atakuwa
amemfunika Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa ambaye kwa sasa
ndiye gumzo miongoni mwa makada waliojitokeza.
Licha ya kuonekana katika skrini hizo, watu wangepa fursa ya kuuliza maswali na kujibiwa papo kwa papo kutoka popote walipo.
Gazeti hili lilikuwa limeshakwenda mitamboni kabla mwanasiasa huyo hajatangaza nia yake.
Kabla ya ubunifu huo, Lowassa alikuwa akishikilia rekodi ya tukio lake la kutangaza nia kwa kujaza watu wengi uwanjani huku maelfu wakifuatilia katika vituo vya televisheni tukio hilo lililofanyika Mei 30, jijini Arusha.
Edward Lowassa.
Januari, ambaye ni mtoto wa Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, mzee Yussuf
Makamba, jana katika Ukumbi wa Mlimani City, alitegemewa kutangaza nia
ya kutaka nafasi hiyo ya juu kisiasa nchini, katika tukio ambalo
lingeonekana pia katika kumbi mbalimbali nchi nzima zilizokuwa
zimeandaliwa na kujaza watu waliomsikiliza na kuuliza maswali ya moja
kwa moja.
Januari Makamba
Akizungumzia kuhusu suala hilo, Makamba alisema kumbi katika mikoa
mbalimbali nchini zilikuwa zimeandaliwa, ambazo zingefungwa skrini kubwa
ambayo watu waliomo wangeweza kumuuliza maswali Makamba akiwa Mlimani
City jijini Dar es Salaam, teknolojia ambayo itakuwa inatumiwa kwa mara
ya kwanza na mwanasiasa nchini tangu Tanzania ipate uhuru wake.Licha ya kuonekana katika skrini hizo, watu wangepa fursa ya kuuliza maswali na kujibiwa papo kwa papo kutoka popote walipo.

Post a Comment