ad

ad

MANCHESTER UNITED YAIKOMALIA REAL MADRID, YASEMA BILA PAUNI MIL 35 DE GEA HAN'GOKI OLD TRAFFORD


Manchester United imetanua mbavu zake kwa Real Madrid na kuwaambia bila pauni milioni 35, hawampati De Gea ng'oo.

United iko tayari kumtumia De Gea kwa msimu mzima ujao na baadae kuodoka bure kuliko kumtoa kipa huyo  kwa bei ya kutupa.

Hatua hiyo inaonekana ni kama ya kulipa kwa Real Madrid ambayo imekataa ofa ya pauni milioni 35 ya Manchester United kumtaka beki Sergio Ramos.

De Gea, 24 aliyejiunga na United mwaka 2011 kwa pauni milioni 17.8 amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake Old Trafford na ataondoka bure kiangazi kijacho.

Ada ya pauni milioni 35 kwa De Gea itakuwa ni rekodi mpya kwa magolikipa duniani, ikivunja rekodi ya Gianluigi Buffon aliyenunuliwa na Juventus kwa  pauni milioni 32 kutoka Parma mwaka 2001.
Manchester United are after a fee in the region of £35million for their goalkeeper David de Gea
Manchester United imeikomalia Real Madrid juu ya usajili wa De Gea 
De Gea is likely to sign for Madrid with Spanish defender Sergio Ramos possibly going to United
De Gea anatakiwa na Madrid huku United nao wakimtaka Sergio Ramos 
United want £35m for De Gea - which would push him ahead of Italy legend Gianluigi Buffon's fee
United wanataka £35m kwa  De Gea -ambayo itamfanya awe kipa ghali zaidi mbele ya Gianluigi Buffon wa Juventus



No comments

Powered by Blogger.