JB:FILAMU ZETU ZINAPENDWA LAKINI HATUNA PESA MFUKONI
MKALI wa filamu za kibongo Jacop Stephen
‘JB’, amefunguka kuwa kazi zao zimekuwa zikikubalika sana na Watanzania lakini
anashindwa kuelewa ni kwa nini bado baadhi ya wasanii wanaishi maisha mangumu.
JB ambaye anaonekana kufanya
vizuri kwenye tasnia hiyo, amesema bado wanachangamoto nyingi za kuangalia
namna na kujikwamua na hali ya umasikini kwa wasanii wa Tanzania.
“Ni lazima tukubali kupapambana
maharamia ambao wanatufanya sisi wasanii kuwa na majina makubwa lakini hatuna
hela, kazi zetu zipo kila kona ya Tanzania zinatazamwa lakini unakuta msanii
huyo huyo maisha yake yanakuwa mabovu wakati mauzo ya kazi zake yanaonekana
kuwa juu,” alisema”.

Post a Comment