ad

ad

MAMIA WALIVYOMZIKA GWIJI WA TAARAB KHAMIS MZINGA



MAMIA ya watu wamejitokeza kumzika Khamis Mzinga, mwimbaji gwiji wa taarab kupitia kundi kongwe la Egptian Musical Club, aliyefariki usiku wa kuamkia leo.

Khamis Mzinga amezikwa katika makaburi ya Tambaza jijini Dar es Salaam saa 11 alasiri ambapo licha ya kuzikwa na watu wengi, lakini wasanii wa taarab walikuwa wa kuhesabika.

Marehemu Khamis Mzinga alijijengea himaya kubwa kwenye muziki wa taarab akiwa mwimbaji bingwa, mtunzi, mtaalam wa kupanga muziki, fundi wa kupiga vyombo kadha wa kadha vya taarab na mwalimu aliyewafundisha muziki wasanii wengi wa taarab.

Lakini marehemu pia kifamilia alikuwa na mzunguko mkubwa uliokaa kitaarab, kama vile; baba yake mdogo, Aboubakar Mzinga aliyekuwa mwanamuziki gwiji wa taraab.
Pia baba yake mzazi, mama yake mzazi wote walikuwa waimbaji wa taarab, huku bintiye Asia Mzinga, mzazi mwenzake, Mwanamtama Amir, shemeji yake Hassan Soud wakiwa ni wanamuziki wa taarab.

Kwa sifa hizo, utaona kuwa Khamis Mzinga alipaswa kuzikwa na wasanii wengi wa taarab wa rika zote, lakini haya siku zote ndiyo yamekuwa maisha ya wasanii wa taarab – kuzikana ni kama dhambi kwao.

Khamis Mzinga amezikwa pembeni ya kaburi la baba yake mzazi pamoja na baba yake mdogo.

Pata picha 25 za mazishi ya Khamis Mzinga yalivyofanyika kwenye makaburi ya Tambaza jirani na hospitali ya Muhimbili.
 Jeneza lililobeba mwili wa Khamis Mzinga likiwasili makaburi ya Tambaza
 Kaburi la Khamis Mzinga
 Baadhi ya wahudhuriaji wakiwa makaburini wa tano kutoka kulia mwenye kanzu ni mkurugenzi wa Melody Ashraf Mohamed
 Jeneza lineza limewasili kwenye kaburi
 Mwili unaingizwa kaburini
 Wahudhuriaji wakiwa kwenye utulivu wa hali ya juu
 Mwili tayari umewekwa kaburini
 Mazishi yanaendelea
 Meneja wa Mashauzi Classic Ismail Sumaragar akishiriki mazishi
  Mpiga kinanda wa  wa Mashauzi Classic (mwenye fulana ya njano) akimwaga mchanga kaburini
 Kushoto ni Aboubakar mtoto wa marehemu Khamis Mzinga akizungumza na mtangazaji wa Magig FM Mwinyiami Maftah
 Wasaa wa kupata kisomo
 Wasaa wa dua, huyu ni mpiga solo wa zamani wa Dar Modern Mridu Ally
Mdau wa taarab Hamad Mmanga
 Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria mazishi ya Khamis Mzinga
Kutoka kushoto ni Feruz mmoja wa maboss wa Ogopa Kopa, mwimbaji mkongwe wa taarab Mustapha Ramadhan na mtangazaji Mwinyiami Maftah "Stazo"
Kushoto ni Sheikh Mohamed Idd akiwa makaburini
Afisa habari wa Simba SC Hajj Manara
Mpiga kinanda Hassan Soud mmoja wa wanafunzi wa Khamis Mzinga
Mheshimiwa Zungu mbunge wa Ilala naye alikuwepo
Umati mkubwa ulijitokeza kumzika Khams Mzinga
Kaburi la Khamis Mzinga (ambalo halijajengewa), mbele yake ni makaburi ya baba yake mdogo na baba yake mzazi 
Kushoto ni Aboubakar mtoto wa Khamis Mzinga 
Ndugu na jamaa wakifanya kisomo baada ya mazishi kukamilika 

CHANZO: SALUTI 5.COM

No comments

Powered by Blogger.