MAINDA AANIKA KINACHOIUA SANAA
BILA kuwataja kwa majina, msanii wa filamu mwenye
Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amesema kitendo cha baadhi ya wasanii
wanaojiona wamefikia vilele vyote vya mafanikio na kuwafanyia roho mbaya
wenzao, ndiyo moja kati ya sababu kubwa zinazochangia sanaa ya uigizaji
kuporomoka.
“Hakuna watu wenye roho mbaya kama wasanii wa uigizaji, kuna ambao wanajiona wamefika vilele vya mafanikio na kwamba hakuna mwingine zaidi yao, hivyo wamekuwa wakiwafanyia fitina wanaokuja kwa kasi kwa kuwapiga majungu, wajiangalie upya na Mungu wa mbinguni awasaidie sana,” alisema Mainda.
Msanii wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’.
‘Akibwabwaja’ na mwandishi wetu hivi karibuni, Mainda ambaye kwa sasa
‘amepangua gia’ zote zenye kasi katika sanaa na kuamua kujikabidhi
madhabahuni kwa Mungu, alisema wasanii wasihangaike kumtafuta mchawi,
badala yake wajichunguze na kujitazama upya kwani wengi wao wana roho
mbaya za kutotaka wengine wapige hatua katika sanaa.“Hakuna watu wenye roho mbaya kama wasanii wa uigizaji, kuna ambao wanajiona wamefika vilele vya mafanikio na kwamba hakuna mwingine zaidi yao, hivyo wamekuwa wakiwafanyia fitina wanaokuja kwa kasi kwa kuwapiga majungu, wajiangalie upya na Mungu wa mbinguni awasaidie sana,” alisema Mainda.
Post a Comment