JOHARI: SIJAFULIA KISANAA
BLANDINA William Wilbert Chagula ‘Johari,’ amesema
kwa sasa amedhamiria kufanya kazi mara kwa mara tofauti na zamani ambapo
alikuwa ‘akibeep’, huku akiweka wazi kuwa waliodhani ameisha kisanii
wakae mkao wa kula kwani alikuwa akiusoma mchezo.
“Nashangaa watu wanasema nimeishiwa kisanii, nilikuwa na majukumu mengine ya kiofisi, lakini sasa narejea tena kwenye umalkia wangu, waliodhani nimefulia kuigiza wakae mkao wa kula,” alisema.
Staa wa filamu za kibongo, Blandina Chagula ‘Johari,’.
Akizungumza kwa njia ya simu na ‘kiruka njia’ wa gazeti hili,
Jumatano ya wiki hii, msanii huyo alisema anasikitishwa sana na maneno
ambayo amekuwa akiyasikia kwa watu wakidai amechuja, wakati ukweli ni
kwamba alisitisha kuigiza kwa sababu alikuwa na majukumu mengine.“Nashangaa watu wanasema nimeishiwa kisanii, nilikuwa na majukumu mengine ya kiofisi, lakini sasa narejea tena kwenye umalkia wangu, waliodhani nimefulia kuigiza wakae mkao wa kula,” alisema.
Post a Comment