JAMANI DADA MARTHA LOOO!-9

ILIPOISHIA:
Penzi ni kikohozi kulificha huwezi, ni kweli kabisa! Licha ya mechi kuihamishia kwenye uwanja wa sebuleni lakini ile wanapuliza kipyenga tu, Martha alianza vuvuzela la mahaba.
“Nyie...nyie kumbe wapo sebuleni kweli lakini si mtu na kaka yake, hebu sikieni,” waliambiana pale nje.
Sauti ya Martha ilisema na kutafsiri kila jambo lililokuwa likiendelea...
“Ooo...” JIRUSHE NAYO SASA...
“Mmm,” aliguna Roi. Hamasa ya mapenzi kwake ilikuwa kubwa sana kiasi kwamba, kila nukta ilikuwa ya furaha kwake.
Kilio cha Martha kilifika nje vizuri sana, wapangaji wenzake wakajisogeza hadi kwenye dirisha la sebuleni na kukaa hapo huku wakijikemea kuwa kimya!
“Ndiyo kaka yake huyu?” mpangaji mmoja aliwaambia wenzake kwa sauti ya chini.
Ilifika mahali, wapangaji hao walitamani kuangalia mechi laivu hivyo wakaanza kuinua vichwa na kusogelea dirishani kabisa lakini pazia lilikuwa madhubuti kutotoa nafasi kuangalia ndani.
Mpangaji mmoja, anaitwa mama Mbega, yeye aliangaza huku na kule na kuona kipande cha mti, akakiokota na kuanza kukipitisha kwenye nyavu, sehemu iliyotoboka. Lengo lake lilikuwa ni kuweka pazia pembeni ili apate nafasi ya kuona mechi inavyoendelea ndani.
“Mh! Jamani tutaonaje sasa ndani?” alisema mama Mbega kwani alishindwa kupenyeza mti kwa kukosa sehemu iliyotoboka.Kelele za Martha ziliwapagawisha wote pale nje. Sasa walikuwa wakihema mihemo kama vile wao ndiyo wako ndani kwenye tukio.
Walishindwa kujizuia mpaka wakaanza kujinyonganyonga huku na kule kwa sababu ya kukumbwa na joto la mahaba ya sauti ya Martha.Martha alisikika kabisa akitangaza nia na kuwafanya wale wa nje kuzidi kuwa moto zaidi...
“Jamani Martha...kwa nini anatufanyia hivi lakini?” wapangaji waliulizana wao kwa wao tena kwa sauti, sema tu Martha na Roi hawakuisikia kwa sababu walikuwa kwenye eneo la mpira wa piga nikupige.
Walipomaliza, wale wapangaji nao wakakimbia. Kila mmoja aliingia ndani kwake na kujilaza kitandani huku wakiugulia maumivu ya joto la mahaba.
“Sweet,” Martha alimwita Roi...
“Niambie.”
“Daa! Afadhali sasa, maana loo...ilikuwa hatari sana,” alisema Martha huku akichekacheka...
“Kwa hiyo sasa umeridhika?”
“Sana tu.”
Wakati Martha anamsindikiza Roi, wale wapangaji walijua, wakatoka kwa mkupuo nje mpaka Martha mwenyewe akashangaa sana...
“Kuna nini kwani? Mbona kama wameibuka kwa mpigo?” alijiuliza Martha lakini hakutoa sauti yake kuwauliza.
“Jamani kaka yangu anaondoka sasa.”
“Oo! Karibu sana kaka.”
“Asanteni sana, siku nyingine.”
“Haya, wasalimie huko, siku nyingine uje hata kama dada yako Martha atakuwa hayupo,” alisema mama Mbega huku akicheka kicheko cha kejeli kama vile moyoni alikuwa akisema...
”Kaka gani wewe Martha, tumesikia kila kitu sisi.”
***
Ulikuwa usiku wa mawazo kwa Martha. Licha ya kwamba alikata kiu yake lakini Martha alijikuta akiumizwa na dhamira mbaya kuhusu Roi...
“Hivi tungebaki kuwa kaka na dada nini kingetokea? Kwanza undugu ungedumu zaidi. Kwa hii hatua tuliyofikia uhusiano wetu utakatika ghafla siku si nyingi,” alisema moyoni Martha akiwa amelala kuangalia juu.
“Ni lazima nichukue uamuzi mgumu. Nimwambie ukweli kwamba tusitishe uhusiano wetu ili ukaka na udada uendelee.”
Alichukua simu, akamtumia meseji Roi...
“Upo?”
Baada ya dakika kumi, Roi alijibu...
“Nipo darling, niambie.”
“Nina jambo linanisumbua, naweza kuchati na wewe kama hutajali?”
“Unaweza baby...”
“Oke. Nimekaa, nimewaza sana. Licha ya kwamba umenikata kiu yangu lakini muda mwingi dhamira inaniambia kwamba tunatakiwa kuendelea kuwa kaka na dada kama makubaliano yetu ya siku ya kwanza kabisa.”
“Mh!” aliguna Roi na ndiyo ikawa jibu lake kwa Martha...
“Usigune Roi, nasema kutoka moyoni mwangu.”
“Mmmh!” Roi alizidisha kuguna, Martha akakasirika na kukaa kimya.
Roi alipoona Martha ametulia, akajua amekasirika, akamtumia meseji...
“Naweza kukupigia?”
“Yes! Unaweza.”
Roi alipiga simu, Martha akapokea haraka sana...
“Halooo...”
“Sista...”
“Yes braza.”
“Umewaza nini tena jamani?”
“Mh! Bro, nimewaza mengi. Mimi nimefikia uamuzi huohuo. Lazima tuendelee kuwa kaka na dada ili uhusiano wetu uendelee kudumu zaidi na zaidi,” alisema Martha...
“Mh! Nikwambie kitu Martha..?”
“Niambie bro...”
Post a Comment