JAMANI DADA MARTHA... LOOO!- 6

ILIPOISHIA
Alikazana sana mpaka Liz akabadili mawazo...
“Bro...oooo...”
“Sist...aaa...”
“Una..unaonaje tukiachana na undugu? Mbona kama huku ni kuzuri zaidi...Broooo...oooo...”JIACHIE MWENYEWE...
“Noo...tuendelee sista...lakini tusirudie tena baada ya leo, tena tujikanye kabisa na tukome kama tulivyokoma kwenye nido za mama zetu, si ndiyo... eee?” alijibu Roi kwa sauti ya kubabaika...
“Bwana...aaa! Mimi sitaki undugu tena kuanzia leo na ufe, kwanza una faida gani kwetu?” alihoji Liz lakini kikubwa kilichoonekana ni tamaa ya mwili iliyombamba kwa wakati huo pale kwenye kitanda...
“Mimi nataka mbona,” aliendelea kusisitiza Roi.
“Ba...aaa...si tumalize kwanza...tu...tajadili.”
Wawili hao, waliendelea kuchekecha mpaka wakacheketuka!
Kwa Liz, moyoni aliamua kuwa, baada ya mechi hiyo, yeye na Roi waendelee kuwa kaka na dada kama walivyokubaliana...
“Si mbaya kama tumeanguka dhambini leo tu, lakini nakuhitaji tuendelee kuwa kaka na dada,” alisema Liz akiwa kwenye kasi ya kupiga mpira kwenye kona karibu na goli!
“Hata mimi ndivyo nitavyotaka. Leo tukimaliza hapa tutubu dhambi zetu, tuanze upya kama kaka na dada, sawa dada angu?” alisema Roi...
“Si sawa...kwa...kwa muda huu tuendelee kuwa wapenzi si mpaka tumalize.”
“Haya.”
Liz alichekecha, akafika mwisho, akatangaza nia na kunyoosha miguu, akatulia tuli huku Roi akijitegemea mwenyewe mpaka naye alipotangaza nia yake.
***
Wote walilala wakiangalia juu huku mazungumzo yao yakiwa ya machalechale. Yalikuwa mazungumzo ya kama ni wapenzi, wakati mwingine kama kaka na dada.
Katika kuonesha kwamba, Liz alijutia kitendo cha kuivunja amri ya sita ya Mungu, aliamua kukaa kitandani badala ya kulala...
“Kaka...”
“Dada...”
“Tutubu dhambi yetu sasa ili tuendelee kuwa kaka na dada kama mwanzoni.”
“Kweli bwana, hebu tubu wewe kwa niaba yangu,” alisema Roi baada ya kuhisi hakuna maneno rasmi ya kutubu...
“Tumwombe Mungu tusirudie tena kufanya dhambi hii, mimi na wewe kuanzia sasa ni kaka na dada tena. Kwa kulitambua hilo naomba tukaoge, tuvae tuondoke,” alisema Liz huku akitoka kitandani. Alikwenda bafuni, akaoga na kurejea, akavaa, akasimama akimsubiri Roi ili waondoke wote...
“Sasa dada wewe umeshavaa, kwa hiyo na mimi nivae mbele yako kama dada yangu?”
“Oo! Ngoja nitoke kaka, nisamehe sana.”
Liz alitoka, akasimama nje ya mlango. Roi alikwenda kuoga, akarudi na kuvaa chapchap, akatoka, akaungana na Liz...
“Dada wewe unaondokea kwa njia gani?”
“Nitapanda Bajaj hapo nje kaka.”
“Oke, basi itabidi tuachane kwa nje au vipi sista?”
“Sawa kaka‘angu.”
Nje ya hoteli hiyo, Roi na Liz waligawana njia, kila mmoja akachukua usafiri wake, wakatawanyika kwa ahadi ya kuwasiliana kwa simu...
“Basi baadaye bro,” alisema Liz...
“Sawa, baadaye dada’angu,” alisema Roi.
Baadhi ya watu walipowaona wanatokea kwenye hoteli hiyo na kuitana dada, kaka walishangaa kwani dalili zote ziliashiria kwamba, wawili hao ni wapenzi.
***
“Ila anajitahidi sana kitandani, hivi kweli tunaweza kuwa kaka na dada maisha yetu yote?” alihoji moyoni Roi...
“Mh! Kaka...kaka kweli! Kaka mzima uwanjani kama Pele...kakaaa...” alisema moyoni Liz akisifia.
***
Ilikuwa usiku wa siku hiyohiyo tu, Roi ndiye aliyeanza kumchokoza Liz...
“Dada Martha mambo?”
Martha aliachia tabasamu kwanza maana alishamwambia mara kadhaa Roi kwamba, asimwite Martha, amwite Liz...
“Kaka Roi,” aliitika kwa kulitaja jina Liz...
“Naam sista...”
“Unalipenda jina la Martha ee?”
Roi ndiyo akashtuka kwamba kumbe alitumia jina hilo...
“Da! Nisamehe sista, kusema ule ukweli nililizoea sana kuliko Lizie...”
“Ona sasa! Siyo Lizie kaka ni Liz...sasa sikia bro, nakuruhusu utumie jina la Martha kuanza leo. Hilo la Liz lifute kabisa kwenye akili yako.”
“Daa! Sista nakushukuru sana mama. Hakuna jina nalipenda kama la Martha kuliko Liz, nashukuru kwa kuniruhusu...”
“Oke usijali baby bro...uko wapi sweetheart kaka?”
“Nipo nyumbani darling sista...”
“Oke! Mtoto mzuri kumbe, wewe ndiye kaka wa kweli.”
“Hata wewe ni dada wa kweli. Good sista...hujalala?”
“Ndiyo nataka kulala sasa. nimechokaaaa!”
“Umechokeshwa na nini sista jamani?”
ITAENDELEA HAPA HAPA
Post a Comment