BEKI WA NIGERIA AANGUKA UWANJANI NA KUFARIKI DUNIA
BEKI wa Nigeria, David
Faramola Oniya mwenye miaka 30 amefariki dunia jana baada ya kuanguka
uwanjani wakati wa mechi ya kirafiki baina ya klabu ya Malaysia Club
T-Team na Kelantan.
Vyombo vya habari vya Malaysia
vinaeleza kwamba nahodha huyo alianguka dakika ya tatu (3) mjini Kota
Bharu na kukimbizwa Hospitalini.
Mkurugenzi wa T-Team, Syahrizan Mohd Zain amesema Oniya alicheleweshwa kupata matibabu ya haraka.
“Alipata shinikizo la moyo
uwanjani, ingekuwa stori nyingine kama dereva wa gari la kubebea
wagonjwa angekuwepo kwa haraka,” Amewaambia New Straits Times.
“Dereva wa Ambulance alikuwa anaangalia mechi wakati Oniya anaanguka ghafla na beki wetu alikosa hewa kwa dakika nyingi”.
Syahrizan amesema mechi ilivunjika dakika ya 60 baada ya kupokea taarifa za kifo cha Oniyo kutoka Hospitalini.
“Alitangazwa kufariki dunia hospitalini baada ya dakika 30″ amewaambia Star newspaper.
Oniya amejiunga na klabu hiyo ya Malaysia msimu huu baada ya kucheza katika nchi za Uzbekistan na Azerbaijan.
Chanzo: Shaffih.com
Post a Comment