Afisa habari wa klabu ya Simba Hajji Manara atoa ya moyoni tuzo za ligi (VPL)
Jana bodi ya ligi kuu Tanzania
bara kwa kushirikiana na wadhamini wao ambao ni kampuni ya simu za
mkononi ya Vodacom, jana walitoa zawadi na tuzo kwa vilabu, wachezaji,
makocha na waamuzi waliofanya vizuri kwenye ligi hiyo iliyomalizika Mei 9
mwaka huu ambapo timu ya Young Africans ‘Yanga’ ilitawazwa bingwa mpya
wa ligi hiyo.
Kumekuwepo na maoni tofauti toka
kwa wadau mbalimbali wa soka juu ya tuzo hizo ambazo zimezua gumzo kubwa
kila kona ya mtaa kwa wapenda soka. Wengi wakidai ni vigezo gani
vilivyotumiwa
Afisa habari wa klabu ya Simba
Hajji Manara ametoa maoni yake ambapo amesema, sio kosa kwa mchezaji
mmoja kuchukua tuzo zaidi ya moja endapo atakuwa anakidhi vigezo lakini
sio vyema kumpa mchezaji au timu flani tuzo kwa lengo la ‘kubalance’
mambo.
“‘Once’ unapochagua mchezaji
bora, kocha bora, timu yenye nidhamu ni lazima kuwe na vigezo. Mchezaji
bora anapatikana kwa vigezo gani, kocha bora kwa vigezo gani, golikipa
bora kwa vigezo gani, mimi sina tatizo na walioteuliwa, nawapongeza sana
kwasababu ndio Vodacom na bodi ya ligi walivyoona”, Manara amesema.
“Lakini hebu waende mbali zaidi
wasiishie hapo, mfano unapomchagua golikipa bora unatuambia amecheza
mechi ngapi, saves ngapi amefanya zinazotambulika. Mfano mzuri ni De Gea
mwaka huu amekuwa golikipa bora wa EPL lakini wanakwambia amechaguliwa
kwasababu moja, mbili, tatu. Kwahiyo unavyomchagua Kado inawezekana
anastahili lakini amecheza game ngapi Kado? Lazima twende beyond that
tusiishie kusema tu”, amefafanua Manara.
Au kwa mfano kakaangu Mbwana
Makata, kuwa best coach wa premier, Je, amefundisha timu yake imeshinda
mechi ngapi kati ya ngapi alizofundisha? Unapowapa Mtibwa timu yenye
nidhamu bora Je, hawa watu hawajapata hata straight red cards?, Je,
hakuna timu ambayo haijapata? Kwamfano sisi Simba hatujapata straight
red card hata moja, wenzetu wamepata mbili lakini sasa ukilalamika
watesema huyu msemaji wa Simba anaitetea Simba lakini sio”, amesisitiza.
“Je, mfungaji bora ni lazima awe
mchezaji bora? Amecheza mechi ngapi na ana assist ngapi? Magoli yake
yamesaidiaje timu yake? Kwahiyo unaweza kusema Msuva anadiserve kwa
vigezo flani tuambie tu. Inawezekanaje ligi ambayo inarundo la foreigner
players ambao huna category hiyo ya mchezaji bora foregner huna.
Unawezaje kuwanyima watu hawa fursa wametoka Uganda, Kenya, Rwanda,
Burundi kwa nini umeshindwa kuwaweka? Huwatendei haki. Halafu hutaki
kuwashirikisha kwenye nafasi ya mchezaji bora wa ligi. Na isiwe dhambi,
kuinyima timu moja au mchezaji mmoja zawadi nne au tano, sio dhambi hata
kidogo kama mtu anastahili apewe yani wasibalance”, amesema.
CREDIT: Shaffihdauda.com
Post a Comment