NDOA YA SHAMSA YAVUNJIKA!...mwenyewe aanika mazito, adai amevumilia weeee!
Mshtuko! Weka pembeni mahaba niue waliyokuwa wakioneshana, staa wa
sinema za Kibongo, Shamsa Ford amefunguka rasmi kuhusu kuvunjika kwa
ndoa yake ya kimila aliyofunga na mwanaume wake wa siku nyingi, Dickson
‘Dick’ akikiri kuwa amepoteza muda mwingi kwa mtu ambaye hakuwa na
mapenzi ya dhati kwake.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Shamsa alitiririka kwamba mara nyingi alikuwa akichezea kichapo tena akiwa na ujauzito wa miezi minne wa mtoto wao, Terry lakini kipindi chote hicho alikuwa akivumilia ili kukwepa aibu na kumlindia heshima.
Alipotafutwa Dick, simu yake iliita bila kupokelewa hivyo jitihada za kumpata zinaendelea.

CHANZO: IJUMAA WIKIENDA
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Shamsa alitiririka kwamba mara nyingi alikuwa akichezea kichapo tena akiwa na ujauzito wa miezi minne wa mtoto wao, Terry lakini kipindi chote hicho alikuwa akivumilia ili kukwepa aibu na kumlindia heshima.
Shamsa Ford akiwa na mumewe wake, Dickson Matoke.
“Dick ameninyanyasa kwa muda mrefu lakini kuepuka aibu ya kuwa
mastaa hawatulii, nikawa navumilia kipigo kikali hivyo niliamua kuachana
naye tangu Oktoba, mwaka jana na sikutaka kusema ila sasa nimeweka wazi
kutokana na yeye kuanika mambo yetu kwenye mtandao wa kijamii,” alisema
Shamsa.Alipotafutwa Dick, simu yake iliita bila kupokelewa hivyo jitihada za kumpata zinaendelea.
CHANZO: IJUMAA WIKIENDA
Post a Comment