ZITTO KABWE: TUHUMA DHIDI YANGU ZICHUNGUZWE
Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe.
Katika
kujitetea mbele ya Baraza la Maadili kuhusu tuhuma dhidi yake za
kugawiwa mgawo wa fedha kutoka akaunti ya Escrow, mbunge wa Sengerema
Bwana William Ngeleja alisema kuwa ni kawaida wabunge kupewa misaada na
wafanyabiashara na taasisi za umma. Katika Maelezo yake alirudia tuhuma
za kipuuzi dhidi yangu zilizokwisha tolewa huko nyuma kwamba
1) nilipewa fedha na kampuni ya PAP na
2) nilipewa fedha na shirika la NSSF.
2) nilipewa fedha na shirika la NSSF.
Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC tunasema “Hatutetereki”
Maelezo yangu kuhusu kazi za Kigoma AllStars/LEKADUTIGITE kwa NSSF na TANAPA. https://www.facebook.com/zittokabwe/posts/755794044441295
MAELEZO BINAFSI YA MHE.
ZITTO ZUBERI KABWE DHIDI YA TUHUMA ZA RUSHWA HUSUSAN KUELEKEA KATIKA
KUPITISHA BAJETI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI
Tuhuma
zote hizo nimewahi kuzitolea ufafanuzi na kukanusha kwani hazina msingi
wowote na zilikuwa siasa za majitaka. Hata hivyo bado zimekuwa
zikijirudia rudia kwa malengo maalumu wanayoyajua wanaotoa tuhuma hizo.
Watuhumiwa wa ufisadi wa escrow hawajazoea kuona taasisi za maadili
zikifanya kazi kwa namna ilivyo sasa na hivyo wanajaribu na watajaribu
kubwabwaja na kuhangaika ikiwemo kutaka kila mtu aonekane ni mtuhumiwa
kama wao. Ndio maana Bwana Ngeleja ametaja msururu wa watu wakiwemo
wafanyabiashara kwamba huwapa fedha wabunge bila chembe ya ushahidi.
Hivyo
narudia kutamka kwamba ninataka uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo ufanyike
mara moja, wenye ushahidi wapeleke kwenye vyombo vya uchunguzi na
niitwe mbele ya Baraza la Maadili kujieleza. Nikiwa mbunge ambaye maisha
yangu yote ya siasa nimeyatumia kupambana na ufisadi na kuchochea
mabadiliko ili kujenga misingi madhubuti ya uwajibikaji na kuimarisha
taasisi zake, nipo tayari kwa uchunguzi mahususi dhidi yangu dhidi ya
tuhuma zilizotolewa na nyingine zozote ambazo mtanzania yeyote anazo
dhidi yangu.
Naunga Mkono kwa
nguvu kubwa kazi inayofanywa na Baraza la Maadili. Ni kazi ambayo
ilipaswa kuwa imefanyika kwa muda mrefu sana kwa kashfa mbali mbali
ambazo viongozi wa umma wamepata kama vile ile ya rada, rushwa katika
manunuzi ya mafuta mazito kuendesha mitambo ya Umeme, kujipatia mikopo
kwenye taasisi za umma bila kulipa, kujilimbikizia Mali tofauti na
kipato nk. Hivyo naiomba Sekretariat ya maadili iyachukue kwa uzito
maoni ya Bwana Ngeleja na kama yana uzito kwa mujibu wa sheria na kanuni
yafanyiwe uchunguzi. Nipo tayari kufanyiwa uchunguzi.
Katika kujenga Misingi Madhubuti ya uwajibikaji nchini ni lazima
kila kiongozi aheshimu taasisi kama Baraza la Maadili. Baraza
likiendelea kufanya kazi kama inavyofanyika sasa, vita dhidi ya ufisadi
itakuwa imepiga hatua na porojo za kuzushiana mitaani zitapungua.
Zitto Kabwe
Mwenyekiti PAC
Dar Es salaam, tarehe 4 Machi 2015.
Mwenyekiti PAC
Dar Es salaam, tarehe 4 Machi 2015.
Post a Comment