MAMA SALMA KIKWETE AKABIDHI MASHINE YA KUPIMIA SARATANI YA MATITI KWA AKINA MAMA HOSPITALI KUU YA JESHI LUGALO
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akikabidhi mashine ya
kupimia saratani ya matiti kwa akina mama kwa uongozi kwa Mnadhimu Mkuu
wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Luteni Jenerali Samuel Ndomba (kulia).
Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika kwenye Hospitani Kuu ya Jeshi
Lugalo kwenye Kitengo cha Uzazi na Mtoto kilichoko Mwenge tarehe
27.2.2015. Aliyesimama pembeni kwa Mama Salma ni Katibu Mkuu wa Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mmbando na aliyesimama kulia kwa
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi ni Mkuu wa Hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugal
Brigedia Jenerali Josia Mwita Makere.
Baadhi
ya viongozi wa Jeshi la Ulinzi na wananchi waalikwa wakisikiliza kwa
makini hotuba ya mgeni Rasmi Mama Salma Kikwete wakati wa hafla ya
kukabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama
Salma Kikwete akitoa hotuba yake muda mfupi kabla ya kukabidhi mashine
ya kupimia saratani ta matiti kwa akina mama kwenye Hospitali Kuu ya
Jeshi Lugalo. Hafala hiyo ilifanyika kwenye Kitengo cha Uzazi na mtoto
cha hospitali hiyo kilichoko eneo la Mwenge hapa Dar tarehe 27.2.2015.
Mnadhimu
Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Samuel
Ndomba akimpongeza Mama Salma Kikwete kwa hotuba yake aliyoitoa kwenye
hafla ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama
kwenye hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugalo tarehe 27.2.2015.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Bibi Mariam Omar aliyemshika
mtoto wake Jane Winston aliyekuwa akisubirim kupata huduma hospitalini
hapo wakati Mama Salma alipotembelea sehemu mbalimbali za Kitengo cha
Uzazi na Mtoto mara baada ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ya
matiti kwa akina mama tarehe 27.2.2015.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akimshauri Ndugu Peter Charles, 28, baba
mzazi wa binti Irene mwenye umri wa miezi 3 na mkazi wa Mikocheni
kupunguza baadhi ya nguo alizomfunika mtoto wakati hali ya hewa ni ya
joto. Mama Salma alimpongeza Ndugu Peter kwa kuambatana na mke wake
kwenda kliniki.
(PICHA NA JOHN LUKUWI)
Kama unapenda kusoma skendo na udaku bofya udaku
ReplyDelete