ad

ad

WATU WANANE WAUAWA KATIKA MILIPUKO TRIPOLI


Watu wanane wauawa katika milipuko Tripoli
Watu wanane wakiwemo raia watano wa kigeni wameuawa leo wakati wanamgambo waliposhambulia hoteli moja ya kifahari katika mji mkuu wa Libya, Tripoli.
Mahmoud Hamza, mkurugenzi wa kikosi maalumu cha kijeshi Libya amesema wanawake wawili ni kati ya raia wa kigeni waliouawa katika hujuma dhidi ya Hoteli ya Corinthia mjini Tripoli. Hata hivyo hakutaja uraia wa watu waliopoteza maisha. Hayo yanajiri siku moja baada ya Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Libya kusisitizia ulazima wa kuwepo askari jeshi wa kulinda amani wa kimataifa nchini humo. Bernardino Leon amesema kuwa ameshauriana na viongozi wa nchi kadhaa kuhusu ulazima wa kuwepo wasimamizi wa kijeshi na kiraia huko Libya, baada ya kufikiwa makubaliano huko Geneva kati ya pande zinazozozana.
Libya imeendelea kushuhudia hali ya mchafukoge na mauaji tangu ulipong'olewa madarakani utawala wa Kanali Muammar Gaddafi, chini ya uungaji mkono wa Jumuiya ya Kijeshi ya Nchi za Magharibi NATO, kiasi cha kupelekea taifa hilo la kaskazini mwa Afrika kuongozwa na serikali mbili na mabunge mawili, huku moja ikiwa haitambuliwi kimataifa.

No comments

Powered by Blogger.