UKARABATI KAITABA STADIUM WAANZA BUKOBA PICHA ZIPO HAPA
Muonekano wa Uwanja wa mpira wa Kaitaba Stadium wa Bukoba baada ya kuanza ukarabati huo tayari Kagera Sugar imeshaomba kutumia Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kwa ajili ya mechi zake za nyumbani.
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema Uwanja wa Kaitaba uliopo mkoani Kagera utaanza kuwekwa nyasi bandia kuanzia Januari 12, mwaka huu.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi alisema kuwa kutokana na ukarabati huo tayari Kagera Sugar imeshaomba kutumia Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kwa ajili ya mechi zake za nyumbani.
Katika hatua nyingine, Malinzi alisema kutokana na kikao cha Kamati ya Utendaji cha Fifa kilichofanyika hivi karibuni, kiliweka bayana kuwa kila mwanachama wa Fifa ataendelea kupata dola za kimarekani 600,000 kwa mwaka kwa ajili ya maendeleo ya soka.
Alisema kiasi hicho kimeongezeka ukilinganisha na mwaka jana ambapo walipewa Dola za Marekani 500,000. Pia, alisema Fifa itatoa dola za Marekani 300,000 kwa ajili ya timu ya Taifa kuanza maandalizi kuelekea kwenye michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika baadaye.
“Fedha hizo zitatolewa ili kuandaa timu zetu za Taifa, kuhakikisha inafanya vizuri katika mchakato wa kutafuta nafasi ya kushiriki kwenye michuano ya Kombe la dunia,” alisema.
Ukarabatiwa Uwanja wa mpira wa Kaitaba Stadium wa Bukoba ukiendelea.
Faustine Ruta wa Bukoba Sports.com akiendelea kutazama ukarabati wa Uwanja huo.
Akionyesha maendeleo ya Uwanja huo.
PICHA ZOTE NA FAUSTINE RUTA - BUKOBA





Post a Comment