ad

ad

FAHAMU NAMNA YA KUANDIKA BARUA YA KUOMBA KAZI



Vidokezo vya namna ya kuandaa barua
bomba ya kuomba kazi
Je ni ipi barua ya kuomba kazi? Ni tofauti
na barua nyingine?
Barua ya kuomba kazi ni tofauti na barua
nyingine. Barua ya kuomba kazi ina
madhumuni ya kukutambulisha kwa
mwajiri mtarajiwa. Hii ni nafasi adhimu
ambayo inabidi itumiwe vizuri. Taarifa zote
zinazokuhusu wewe ni muhimu zikawepo
katika barua hii ili kuweza kumshawishi
mwajiri mtarajiwa. Hakikisha unaweka
ujuzi, taaluma na uzoefu ulionao ambao
utakufanya wewe kua mtahiniwa
unaehitajika kujaza nafasi iliyopo. Hizi ndio
taarifa ambazo Waajiri huangalia
wanaposoma barua yako.
Ni kwanini unatakiwa kuambatanisha barua
pamoja na CV wakati wa kuomba kazi?
Barua hii huwekwa kwa madhumuni ya
kujitambulisha kwa mwajiri mtarajiwa kwa
kuzingatia nafasi uiombayo. Kwa kawaida
taarifa unazoziweka katika barua hii hua ni
kama kujitangaza mwenyewe na sifa zako
na kwa namna gani sifa na ujuzi ulionao
utakusaidia katika kufanaya kazi
unayoiomba. Barua hii ikiandikwa vizuri
humpelekea mwajiri kupitia CV yako kama
hatua nyingine.
Ni wakati gani na ni wapi utume barua
yako?
Barua hii huitajika pale ambapo nafasi ya
kazi hua imetangazwa. Hata kama tangazo
la kazi halijakutaka uandike barua hii, siku
zote ni vizuri na huongeza uzito kama
itaambatanishwa na CV. Barua hii ni
tangazo kuhusu wewe, ni vizuri ukaiandika
katika namna ambayo itakuuza vizuri
katika soko la ajira.
Vile vile unaweza kutuma barua ya kuomba
kazi isiyokua mahsusi kama mawakala wa
kuajiri (recruitment agent) hawajatangaza
kazi. Katika hali kama hii jitahidi barua
yako iwe na taarifa zote muhimu ambazo
zitakusaidia kupata kazi. Ni kama unatuma
barua katika jopo la Waajiri ambao kila
mmojawapo ana vitu vyake anavyovipenda
hivyo ni vizuri ukajielezea kiundani zaidi ili
kuwapa fursa ya kukuona wewe katika
muonekanao tofauti tofauti. Kila barua ni
vizuri ikaandikwa kwa kuzingatia mahitajai
ya kazi iombwayo.
Kuomba kazi bila kuona tangazo la kazi
Wakati mwingine unaweza kuamua
kuandika barua ya kuomba kazi katika
kampuni Fulani hata kama hawajatangaza
kazi. Kitu cha muhimu ni kuandika barua
hiyo kwa kuzingatia mahitaji ya mwajiri
unaemlenga.
Uandishi wa barua hii ni tofauti huanza kwa
kufanya tafiti inayojitosheleza katika
kampuni unayoilenga. Lengo likiwa ni
kufahamu majukumu, itikadi na malengo ya
kampuni husika ambayo yatakusaidia wewe
kuandika barua yenye mvuto na
inayoendana na mahitaji ya kampuni. Vile
vile barua yako ni vizuri ikaomba kukutana
na mwajiri kwa ajili ya majadiliano zaidi,
kama vile kuombwa kuitwa kwenye usahili.
Hakikisha mara zote unaonyesha ujuzi na
utaalamu unaohitajika, mwajiri
hatokuchagua wewe dhidi yaw engine
wengi kwasababu ya kiingereza chako
kizuri, uzuri wako lakin atakuchagua
kwasababu ya ujuzi ulionao unaohitajika
katika kazi. Ni muhimu kuhakikisha kua
kila unapokutana na mwajiri mtarajiwa
unaonyesha ujuzi na utaalamu ulionao ili
kukurahisishia kupata kazi.
Ni ipi njia muafaka ya kutuma barua yako?
Katika hili hakuna unashauriwa utumie njia
amabayo ni rahisi na nafuu kwako. Kwa
kuzingatia maendeleo ya teknolojia, mfumo
wa barua pepe ni njia muafaka na nafuu
zaidi kutuma barua hizi. Hakikisha
unafuata mahitaji yote muhimu ya kuandika
barua maalumu wakati wa kuandika barua
ya kuomba kazi. Vile vile hakikisha kua
ujuzi na uzoefu wote ulioweka katika barua
yako pia upo katika CV yako ambayo
utaiambatanisha na barua hiyo. Ukitekeleza
haya utakua na nafasi kubwa ya kuitwa
kwenye usahili. Ukiitwa kwenye usahili
hakikisha unafahamu vidokezo muhimu
vya kuzingatia wakati wa usahili.

No comments

Powered by Blogger.