UGOMVI KATI YA AMISI TAMBWE WA YANGA NA BEKI WA RUVU SHOOTING, GUMZO KWA WANAMICHEZO
GUMZO linaendelea kwa sasa kwenye soka la ugomvi wa uwanjani kati ya Mrundi Amissi Tambwe wa Yanga na beki wa Ruvu Shooting, George Michael ambaye ni askari.
Ingawa tatizo lao limeonekana jipya baada ya picha ya Michael akimkaba shingoni Tambwe kuchapishwa kwenye Gazeti la Championi juzi Jumatatu, ukweli ni kwamba ‘uadui’ wa wawili hao ulianza tangu Tambwe akiwa straika wa Simba msimu uliopita.
Michael alimkaba Tambwe katika mechi hiyo ya Jumamosi hadi kumuumiza mdomo na jicho, hali ambayo imefanya wadau wengi walaani.Lakini ugomvi huo unathibitishwa na rekodi kwamba tangu msimu uliopita, Tambwe aliifunga Ruvu mabao matatu katika mechi mbili za ligi.
Oktoka 5, 2013 katika mechi ya msimu wa 2013-14, bao moja la penalti, Michael akiwa uwanjani lakini akafunga mawili tena katika mzunguko wa pili matokeo Simba ikishinda kwa mabao 3-2. Wakati huo Michael alikuwa anauguza majeraha ya kuvunjika mguu.
Katika mechi hiyo ya kwanza, Michael alimuumiza Tambwe jichoni na kumaliza mechi akiwa na nundu chini ya jicho lake la kulia.Tambwe ameeleza kuwa kweli beki huyo amekuwa akimchezea ‘kindava’ tangu akiwa Simba msimu uliopita alioibuka mfungaji bora akiwa na mabao 19.
“Hii siyo mara ya kwanza, yaani huu ndiyo umekuwa mchezo wake kila tukikutana, anafanya faulo zisizo za kimpira. Wakati nikiwa Simba msimu uliopita kwenye mechi ya pale taifa, alinichezea sana rafu mpaka nikawa nashangaa, aliniumiza jicho.
“Lakini sasa nimekutana naye pia nikiwa Yanga, nashangaa amekuwa na mchezo uleule, tena safari hii akiwa amezidisha kabisa yaani imekuwa si sahihi kwa jinsi anavyofanya, kila mtu ameona kupitia picha za Gazeti la Championi.
“Kuhusu adhabu, sasa ni jukumu lao TFF (Shirikihso la Soka Tanzania) kuangalia wanadhibiti vipi hali hii, kwa sababu wenyewe wameona pia,” alisema Tambwe.
Pia rekodi zinaonyesha beki huyo amewahi kuwachezea kindava kweli Hamisi Kiiza wakati akiwa Yanga pamoja na Ramadhani Singano ‘Messi’ wa Simba.Juhudi za kumpata Michael zilishindikana kutokana na simu yake kuwa imezimwa siku nzima ya jana.
CHANZO: CHAMPIONI JUMATANO

Post a Comment