ad

ad

SSERUNKUMA AONGOZA KWA KUOTEA UWANJANI


MSHAMBULIAJI wa Simba, Mganda, Dan Sserunkuma, ameweka rekodi ya pekee katika michuano ya Kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kufikia tamati kesho baada ya kuongoza kwa kuotea uwanjani.
Sserunkuma ambaye alijiunga na Simba hivi karibuni akitokea Gor Mahia ya Kenya, tangu kuanza kwa mashindano haya, ameotea mara 18.

Mchezaji huyo amejikuta akifanya hivyo akiwa katika harakati za kuhakikisha anapata bao ili aweze kuondokana na hali ya sasa ambayo inausumbua ubongo wake ya kutofunga bao lolote tangu ajiunge na timu hiyo.

Jambo hilo limekuwa likimuumiza kichwa kila wakati, hivyo kujikuta akitafuta bao kwa udi na uvumba lakini bila ya mafanikio.Katika mechi ya nusu fainali ya michuano hiyo ambayo Simba ilicheza dhidi ya Polisi juzi, Sserunkuma aliotea mara nane wakati katika mechi ya robo fainali dhidi Taifa Jang’ombe, aliotea mara nne.

Mbali na mechi hizo pia aliotea mara tatu timu hiyo ilipocheza na Mtibwa Sugar katika hatua ya makundi, mara mbili dhidi ya JKU na mara moja dhidi ya Mafunzo.

No comments

Powered by Blogger.