KOCHA SIMBA AFANANISHWA NA MR BEAN
WAKATI michuano ya Kombe la Mapinduzi ikiwa tayari imetinga hatua ya fainali, Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic, amezawadiwa jina jipya la Mr Bean visiwani hapa.Hatua hiyo imetokana na vituko vyake anavyoonyesha wakati timu hiyo inapokuwa ikicheza.
Jina hilo la Mr Bean ni la mchekeshaji raia wa England, Rowan Atkinson.
Kopunovic amekuwa burudani tosha kila timu yake inapocheza ila zaidi ilikuwa katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Polisi Zanzibar, juzi Jumamosi.
Katika mechi hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Amaan na Simba kushinda bao 1-0, kocha huyo alikuwa burudani ya pekee iliyowafanya mashabiki wa visiwani hapa wamfananishe na Mr Bean kutokana na vituko vyake.
Mara kwa mara alionekana akirusha mikono yake juu, akipiga makofi, akipiga chenga bila kuwa na mpira, akiruka juu bila ya kuongea lolote, jambo ambalo lilifanya baadhi ya wapenzi wa soka uwanjani hapo kumuangalia yeye tu muda mwingi.
Post a Comment