ad

ad

KOCHA MKUU WA YANGA, MHOLANZI, HANS VAN DER PLUIJM



KOCHA Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, amemvaa mshambuliaji wake Mrundi, Amissi Tambwe, akimwambia yeye anataka mabao tu na siyo kingine.

Tambwe alijiunga na Yanga kwa mkataba wa mwaka mmoja kwenye usajili wa dirisha dogo akitokea Simba, lakini amefunga bao moja tu akiwa Jangwani huku akishindwa kupachiba bao lolote wakati Yanga ikiaga kwenye michuano ya Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar.

Akizungumza Pluijm alisema anaujua vizuri uwezo wa Tambwe akiwa anaichezea Simba, hivyo alishangaa kuona akikosa nafasi nyingi za wazi katika mechi alizocheza kwenye Kombe la Mapinduzi.

Pluijm alisema anaheshimu kiwango cha mshambuliaji huyo alichokiona msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara akiwa na Simba akitwaa ufungaji bora, hivyo anataka kuona akibadilika kwa kufunga ili kufanikisha ushindi katika ligi kuu na mashindano mengine.

“Mimi ninataka kuona kazi ndani ya uwanja na siyo kingine, kama mshambuliaji jukumu lake linatakiwa kufunga mabao na siyo kingine.“Ninatarajia kuona Tambwe akifunga mabao ndani ya uwanja kutokana na umahiri wake mkubwa wa kufunga mabao, nilimuona akiwa na Simba ni mchezaji mwenye uwezo, kikubwa anachotakiwa ni kupunguza presha aliyonayo.

“Ninakubali na kuheshimu uwezo wake, hivyo sina cha kuongea zaidi, acha nimuangalie kwenye mechi za ligi kuu, ninaamini atafunga mabao mengi,” alisema Pluijm.

No comments

Powered by Blogger.