Askari JWTZ Walionusurika Shambulio la DRC Wanaendelea Vizuri – Pichaz
Miili ya wanajeshi waliouawa kwenye shambulio hilo iliagwa juzi Desemba, 14 mwaka huu katika Viwanja vya ulinzi vilivyopo makao ya jeshi yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya Wanajeshi wa JWTZ waliojeruhiwa kwenye shambulio nchini DR Congo
wakiwa kwenye hospitali ya Goma ambapo wanaendelea kupatiwa matibabu.
Mkuu
wa operesheni za ulinzi za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix
amewajulia hali walinda amani wawili wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) waliolazwa katika hospital ya Mulago mjini Kampala
nchini Uganda.

Askari hao 14 walifariki dunia katika mapigano na waasi wa kikundi cha ADF nchini DRC, huku 44 wakijeruhiwa na mmoja akipotea baada ya kambi yao kuvamiwa eneo la Mashariki mwa nchi Desemba 7 wakati wakitekeleza majukumu ya ulinzi wa amani.

Post a Comment