PHIRI, MATOLA WAWAGOMBANISHA VIONGOZI SIMBA
SAKATA la kuondolewa kwa benchi la ufundi la Simba,
lililokuwa likiongozwa na Mzambia, Patrick Phiri limechukua sura mpya,
baada ya viongozi kutofautiana kauli kuhusu kubadilishwa kwake.

Mapema wiki iliyopita, uongozi wa Simba ulisitisha kibarua cha Mzambia huyo na nafasi yake kuchukuliwa na Mserbia, Goran Kopunovic, hata hivyo wapo kwenye mpango wa kumuondoa pia msaidizi wake, mzawa, Selemani Matola.
Kitendo cha kutaka kumuondoa Matola ambaye anatajwa kupelekwa kwenye timu ya vijana, kimeleta tafrani ambapo jana kulikuwa na kikao kizito ambacho kiliaminika kilikuwa kikijadili suala la kumuondoa Matola na nafasi yake inatajwa kuchukuliwa na Mnyarwanda, Alphonce Gatera, lakini baadaye suala hilo waliamua kuliachia kamati ya usajili.
Inasemekana kuwa Mserbia huyo alimpendekeza Gatera kuwa msaidizi wake kwani waliwahi kufanya kazi wote katika Klabu ya Polisi ya Rwanda.
Habari za ndani kutoka Simba zilizolifikia Championi Jumamosi, zilidai kuwa baadhi ya viongozi wanapinga ujio wa Mnyarwanda huyo huku wakitaka afanye kazi na Matola kwa kuamini kuwa Phiri ndiye alikuwa tatizo, lakini wapo ambao wanataka benchi zima ‘lisafishwe’.
“Kwa hiyo mpaka sasa (jana) jioni, hakuna muafaka kamili kuhusu ujio wa kocha huyo kutokana na pande mbili kukinzana,” kilisema chanzo chetu na kingine kuongeza kuwa;
“Sisi tulipendekeza Matola abaki, kwa hiyo kama huyo mwingine anatafutwa leo hii, sijui wamepanga vipi,” alisema mmoja wa viongozi wa ngazi za juu.Championi ilipowatafuta rais na katibu wa klabu hiyo, Evans Aveva na Stephen Ally kwa nyakati tofauti, wote walisema kuwa bado wapo kwenye mchakato kuhusu suala hilo.
“Kwa sasa akili yetu tumeiweka kwa kocha mkuu (Kopunovic), kwa hiyo suala hilo halijajulikana, hivyo siwezi kuzungumzia ujio wake,” alisema Rais Aveva huku Katibu Ally akisema: “Naomba suala hilo liache kwanza maana bado kuna mchakato kidogo na mazungumzo yahajakamilika.”
Wakati huohuo, baadhi ya wanachama wamepinga kuondolewa kwa Phiri wakisema kuwa hakupewa muda wa kutosha katika kuijenga timu hiyo na kupinga maamuzi walioyaita ya kukurupuka.
CHANZO: CHAMPIONI JUMAMOSI

Post a Comment