HATIMAYE MWILI WA ASIHA MADINDA WAFANYIWA UCHUNGUZI MUDA HUU, MAZISHI NI LEO MCHANA
Baada
ya danadana nyingi, hatimaye mwili wa mnenguaji Aisha Madinda
unafanyiwa uapasuaji muda huu katika hospitali ya Muhimbili, jijini Dar
es Salaam.
Akizungumza
na Saluti5, mkurugenzi wa Aset Asha Baraka amebainisha kuwa upasuaji
umeanza dakika 10 zilizopita na ni zoezi linalotarajiwa kuchukua masaa
mawili.
Asha
Baraka amesema baada ya zoezi hilo, watauosha mwili wa marehemu katika
msikiti ulioko hapo Muhimbili ikiwa ni pamoja na uvishaji wa sanda kabla
ya kuelekea nyumbani kwao Kigamboni.
Mazishi ya Aisha Madinda yatafanyika Kigamboni makaburi ya Kibada leo mchana muda wowote baada ya sala ya Ijumaa kutegemea na namna zoezi la Muhimbili litakavyokamilika mapema.
Upasuaji
wa mwili wa Aisha Madinda ulitarajiwa kufanyika tangu saa 1 asubuhi,
lakini wakati daktari akiwa ameshafika, polisi aliyetakiwa kusimamia
zoezi hilo akachelewa kufika.
Ilibidi
Asha Baraka aende hadi kituo cha polisi cha Oysterbay kuonana na polisi
aliyetakiwa kusimamia uchunguzi wa Aisha Madinda na ndipo askari huyo
akaondoka kuelekea Muhimbili.
Upasuaji
huo ulishindikana jana mchana kwa madai ya kuwa muda wa kufanya
upasuaji umekwisha na kama si juhudi za Asha Baraka basi hadithi ya jana
ingejirudia tena.
CHANZO: SALUTI5.COM, SAID MDOE
Post a Comment