FABREGAS AZIDI KUMUUMBUA WENGER
KIUNGO, Cesc Fabregas anazidi kumuumbua kocha wake wa zamani,
Arsene Wenger ambaye alipuuza kumsajili katika kipindi cha usajili cha
majira ya kiangazi mwaka huu.
Wenger anayeinoa Arsenal alikuwa wa kwanza kupewa nafasi ya kumsajili kiungo huyo huku mwenyewe akiwa tayari kurejea katika klabu yake hiyo ya zamani baada ya kuamua kuachana na Barcelona, lakini Mfaransa huyo alipuuza na kudai kwamba kikosi chake kina viungo wengi wanaocheza nafasi yake akiwamo Jack Wilshere.
Fabregas aliamua kutua Chelsea, mahali ambapo amekuwa moto msimu huu kwa kuifanya timu hiyo kutamba kwenye Ligi Kuu England na kushika usukani wa ligi hiyo.
Mambo anayoyafanya Fabregas klabuni Chelsea yamewatia hasira mashabiki wa Arsenal na kumshangaa kocha wao kwa nini alimpuuza kumsajili Mhispaniola huyo kwa kung’ang’ania viungo wake aliokuwa nao ambao wengi wamekuwa wakisumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara akiwamo Mesut Ozil.
Akiwa kwenye jezi za Chelsea msimu huu, Fabregas amepiga pasi 16 zilizozaa mabao katika mechi zake 12 alicheza kwenye Ligi Kuu na kumfunika Wilshere aliyepiga pasi 11 katika mechi 95 alizochezea Arsenal tangu alipopandishwa kwenye kikosi cha kwanza.
Post a Comment