ad

ad

KOCHA MOURINHO ASEMA NI NDOTO LIONEL MESSI KUTUA STAMFORD BRIDGE

MAISHA yanaenda kasi sana. kama jaribio la aliyekuwa mwanasoka bora wa dunia kwa miaka minne mfululizo lingeweza kufanikiwa, leo mashabiki wa Arsenal wangekuwa wanakenua meno na kutamba mitaani.

 

Inadaiwa kuwa staa wa Barcelona, Lionel Messi alitaka kufanya uhamisho wa kushangaza kwenda Arsenal miezi miwili iliyopita kabla hajaamua kusaini mkataba mpya na Barcelona ambayo alikuwa ameyumbishana nayo kipindi kirefu.

Staa huyo wa kimataifa wa Argentina ambaye ameng’ara na kikosi cha nchi yake nchini Brazil katika michuano ya kombe la dunia alisaini mkataba mpya na Barcelona Mei mwaka huu baada ya kukataa baadhi ya vipengele hasa vinavyohusu posho.

Kwa mujibu wa gazeti la Hispania, Vozpopuli, ambalo ndilo lilikuwa la kwanza kuandika habari za Alexis Sanchez kutua Arsenal, lilisema kwamba Messi alikuwa amejikita katika kuhamia Arsenal kabla ya kumaliza matatizo yake na Barcelona.

Gazeti hilo linadai kuwa Messi alikuwa ameongea na rafiki yake wa karibu, Cesc Fabregas akimuulizia maisha ya Arsenal na pia alimuweka wazi kwamba angependa kuhamia katika timu hiyo yenye makazi yake jiji la London.

Inaeleweka kwamba Messi alimwambia wakala wake aangalie kwa uhalisia kama kuna uwezekano uhamisho wa kwenda Arsenal unaweza kufanyika lakini kabla jambo hilo halijafanyiwa kazi Barcelona ilifanikiwa kumalizana na nyota huyo mwenye umri wa miaka 26.

Kutokana na mkataba wake wa sasa unaotarajiwa kumalizika Juni 2018, Messi analipwa euro 16 milioni kwa mwaka akiwa ni mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani kwa sasa kando ya Cristiano Ronaldo.

Messi alikuwa na nafasi ya kujiunga na Arsenal angali akiwa mtoto kabla ya Barcelona kuchukua nafasi hiyo kumpeleka katika shule yao ya soka maarufu kama La Masia akijiunga na makinda wengine kama Fabregas na Andres Iniesta.

Ingawa amekuwa akiwindwa vilivyo na timu zenye utajiri mkubwa wa pesa za mafuta kama PSG na Manchester City, inadaiwa kuwa Messi ni shabiki mkubwa wa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger huku akivutiwa na kandanda la mabingwa hao wa michuano ya FA.

No comments

Powered by Blogger.