ad

ad

USIKU WA KIGODORO - 07


Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com

ILIPOISHIA :Lina alifika hotelini, akasukuma mlango na kuzama kwenye chumba alichomo mume wake wa pili James.
“Hodi.”
NING’INIA NAYO…
James alifungua mlango, ukawa wazi mpaka mwisho. Lakini alionekana kukunja sura na kupoteza uchangamfu kuliko siku nyingine.
“Karibu.”
Lina aligundua James hakuwa sawa…
“Baby kama haupo sawa, kuna nini?”
“Lina, mimi ni nani kwako?”
“Mume wangu.”
“Unatakiwa kumsikiliza dada ‘ako au mimi?”
“Wewe.”
“Basi naomba unisikilize kuanzia sasa.”
“Kwani sikusikilizi baby? Mbona mimi nakusikiliza sana jamani.”
“Lakini si kwa kiwango kinachotakiwa Lina, ongeza usikivu wako kwangu. Mbona mapema sana kuanza kuonesha si msikivu!”
“Nisamehe mume wangu.”
“Oke, yamepita nakupenda sana.”
“Asante baby, nakupenda pia.”
Walikumbatiana wakaganda kwa muda huku kila mmoja akimtazama mwenzake machoni, mwishowe wakaachia tabasamu laini, wakapanda kitandani ambako Lina ndiye aliyeanzisha kupeana muwashawasha kwa James naye akapokea, wakakukuruka mpaka wakaingia uwanjani kuanza mchezo.
***
Usiku uliingia, Lina alikuwa akipiga mahesabu ni uongo  gani atamwambia mume wake akaeleweka ili asirudi nyumbani siku hiyo. Kwa siku hiyo kumpigia asingeweza maana muda wote James alikuwa yuko naye beneti. Akaamua kutuma meseji.
“Baby, hali ya dada’ke Eg bado si nzuri. Naomba nilale hospitali maana naye Eg ana mgonjwa mwingine pale kwake.”
Baada ya kutuma meseji hiyo, kila sekunde Lina alikuwa akiiangalia simu yake ili kuona kama meseji ya majibu itaingia.
Zilikatika dakika kumi meseji yake haijajibiwa, mwishowe akaanza kuingiwa na wasiwasi kwamba huenda mume wake hajapenda ruhusa hiyo na kama ndivyo, ataagaje kwa James ili arudi nyumbani. Mara, meseji ya mume wake Semi iliingia.
“Sijakubaliana na wewe, Eg aangalie utaratibu mwingine wa mtu wa kulala na mgonjwa wake na si wewe.”
Ni kujikaza tu, lakini Lina alibadilika rangi muda uleule ila alijichangamsha ili kutompa nafasi James kumsoma. Moyoni alijua kuna ugumu mkubwa kwa James kumkubalia aondoke. Kwanza atasema anakwenda wapi?
“Mh! Nimeyavulia nguo mwenyewe, lazima niyaoge sasa,” alijisemea moyoni huku akianza kutetemeka mpaka James akajua.
“Vipi baby mbona kama unatetemeka?”
“Wala, niko fiti tu.”
Kwa mbali Lina alipata akili kwamba, amtumie meseji Eg na kumwambia apige simu kwake aseme kuna shangazi mgonjwa amepelekwa Muhimbili muda huo, awahi Muhimbili.
Baada ya kujiridhisha kwamba itakuwa sawasawa, Lina alituma meseji hiyo kwa Eg ambaye alijibu kwa ufupi poa! Lakini akatuma nyingine akimuuliza apige simu au atume meseji?
“Piga kabisa,” alijibu Lina.
Alijifanya anakwenda chooni ili simu ya Eg ikiingia ipokelewe na James na ikibidi ujumbe huo upokelewe na yeyeyeye James.
Ile anafika chooni tu, simu yake ikaita. James akatupa jicho kwenye skrini, akasoma jina akamwita Lina.
“Baby…”
“Abee…”
“Kaka Semi.”
Kaka Semi ni mume wa Lina. Wakati anakwenda hotelini hapo aliamua kubadii jina la mume wake, badala ya kuandika My Huzband kama ilivyokuwa mwanzo, akaandika kaka Semi akiamini kwamba  anaweza kupiga wakati yeye yupo na James itakuwa soo kuonekana My Huzband!
Lina alitoka mbio huku mapigo ya moyo yakimwenda kasi kwa sababu hakutegemea kama  mumewe angepiga simu muda ule.
Lina aliipokea simu kutoka kwenye mikono ya James akiwa haamini maana alijua kuwa hata kama James angeamua kupokea na kusema ‘mwenye simu yuko mbali’ au ‘subiri kidogo’ ingekuwa soo kwake.
Pia alijua kuwa, James angeweza kuipokea simu hiyo kwa lengo la kusalimiana na shemeji yake huyo aitwaye Semi kwa mujibu wa jina la kwenye skrini ya simu.
Lina alijifanya anaipeleka simu hiyo sikioni huku akiikata halafu akajifanya anaongea.
“Shikamoo kaka Semi…mimi sijambo, za huko? Hawajambo wote? Sisi tunaendelea vizuri, utakuja lini? Haya karibu sana, shemeji yako utamuona tu ukija, yupo! Haya kwa heri kaka.”
Alipomaliza kusema kimagirini, alituma meseji kwa mumewe.
“Kuna daktari kapita wodini, nitakupigia. Lakini pia nitakuja nilikuelewa.”
Alichokitaka Semi ni hicho kujua kwamba,  kukataa kwake Lina asilale hospitali alielewa. Mara, ikaingia simu ya Eg, Lina akiwa amesimama dirishani, James akatupia tena macho na kumwambia...
“Eg anapiga, ngoja nipokee nimsalimie…shemeji mambo? Ee…yupo…nani? Amelazwa..? Hospitali gani? Hebu ongea na Lina huyu hapa shemeji…”

“Haloo…amelazwa? Anaumwa nini? Oke, nakuja basi.”
Lina alikata simu na kumgeukia James…
“Vipi?” aliuliza James…
“Mh! Majanga… itabidi niende hospitali.”
“Ameniambia aisee. Da! Sasa si itabidi nikupeleke?”
“Utanipeleka? Si ulisema unapenda wiki nzima ushinde ndani tu!”
“Ni kweli, lakini sasa wewe utaendaje?”
“Nitachukua Bajaj…”
“Kwanza leo nataka kukwambia jambo, mambo ya kupandapanda Bajaj yaishe, sitaki kuona. Nitakununulia gari tukimaliza fungate, kwa hiyo itabidi ujifunze kuendesha…ila leo nenda na teksi,” alisema James huku akimwagiza Lina kutoa pesa kwenye brifkesi…
“Nichukue shilingi ngapi?”
“Unayoona inatosha.”
Lina alitumbukiza mkono akaibuka na shilingi elfu hamsini…
“Nimechukua hamsini.”
“Sawa, kawape pole wote.”
Lina alichukua Bajaj hadi nyumbani kwake ambapo alimkuta mumewe, Semi. Swali la kwanza alilokumbana nalo kwa mumewe ni kuhusu pete ya ndoa na ya uchumba…
“Baby, hivi hizo pete ulizipeleka tena kwa sonara nini, maana naziona zinang’aa sana siku mbili hizi.”
“Nilipeleka zikaoshwa. Niliona zimeanza kuingia giza.”
“Oke, zimekuwa nzuri sana,” alisema Semi bila kujua kwamba zile ni pete mpya ambazo alizinunua James kwa ajili ya ndoa hiyo.
***
 Lina amefika kwake, kazi ikawa kumsikilizia James akipiga kuulizia kuhusu mgonjwa. Aliumia sana moyoni kiasi kwamba alitamani kumwandikia meseji amwambie ukweli kwamba yeye ni mke wa mtu, tena kwa ndoa lakini kila alipofikiria kuhusu hilo akiamini hata James alifunga naye ndoa alikosa la kufanya.
Eg alimpigia simu Lina na kumuuliza kama dili lao lilitiki au la! Alipoambiwa limetiki, akacheka sana na kukata simu huku moyoni akisema…
“Lakini sisi tuna hatari sana. Ni kweli Lina ataweza kudumu na James kwa muda mrefu bila kujulikana? Sidhani aisee!”
***
Saa kumi na mbili jioni, Lina akiwa chumbani simu yake iliita. Na muda huo aliamua kwa makusudi kuwa chumbani akijua lazima James atapiga…
“Haloo,” alipokea kwa sauti ya chini, mume wake alikuwa amekaa sebuleni…
“Vipi mgonjwa?”
“Mgonjwa hali mbaya James, hivi hapa daktari ndo ameingia sasa hivi.”
“Mh! Sasa itakuaje? Ahamishwe hospitali.”
“Sijajua ndugu watasemaje maana waliondoka na hawajarudi. Hivi nilitaka kukwambia naomba nilale nitoke asubuhi kuja huko.”ITAENDELE KESHO.
“Sawa, lala tu Lina, wale wakija asubuhi wewe unatoka, si ndiyo?”
“Ndiyo.”
“Basi hamna shida.”
Lina alijisikia furaha ya aina yake, kwani alijua amemaliza kazi kubwa sana ya siku hiyo…
“Kibarua cha leo kimeisha, bado cha kesho, keshokutwa, mtondogoo na siku za mbeleni, sijui itakuwaje!”
***
Asubuhi ya saa kumi na mbili, Lina alitoka na simu yake hadi uani, akampigia simu James haraka ili arudi tena kitandani kulala…
“Umeamkaje baby?”
“Nimeamka poa. Vipi mgonjwa?”
“Mgonjwa hivyohivyo tu, hakulala usiku.”
“Da! Poleni sana. Wameshakuja hao?”
“Wako njiani, watafika kwenye saa mojamoja hivi, maana watashinda hapa.”
“Sawa. Sasa ukitoka si unakuja huku?”
“Yeah!”
“Oke poa.”
“Oke, baadaye basi.”
***
Asubuhi ya siku hiyo, Lina alipotoka kuoga na kuvaa ili aende kwa James alipata wakati mgumu kwani isingekuwa kawaida aende akiwa amevaa nguo nyingine wakati James anajua alikwenda hospitali. Lakini pia isingekuwa rahisi avae nguo zilezile mbele ya mume wake. Kwa siku hiyo, mume alijua anakwenda kazini.
Ilibidi avae nguo nyingine, akazichukua za jana yake na kuzitia kwenye mkoba na kuondoka zake.
“Mume wangu baadaye.”
“Sawa, kazi njema.”
“Poa.”
Nje, Lina alichukua Bajaj na kwenda hotelini kwa James. Lakini alimshangaza sana dereva wa Bajaj kwani walipokaribia nje ya hoteli, alimwambia suka huyo asimamishe Bajaj na afungue turubali ili abadili nguo, avae ileile ya jana yake kisha zile alizovaa siku hiyo akaziweka kwenye mkoba…
“Kwani vipi anti, sijakuelewa?”
“We acha tu. Nina mambo makubwa sana, usinione hivi.”
“Mambo gani, siwezi kukusaidia mimi?”
“Huwezi.”
Mara, simu yake ikaita, mumewe alipiga…
“Nakuja hapo ofisini kwako, kuna mzigo nataka kuuacha,” akakata simu.
  

No comments

Powered by Blogger.