SIKU YA MSANII YAFANA USIKU WA KUAMKIA LEO MLIMANI CITY, DAR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiongea jambo usiku wa kuamkia leo Mlimani City katika Siku ya Msanii.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia akiongea na wasanii katika Siku ya Msanii.
Dkt. Mohammed Gharib Bilal akikabidhi tuzo kwa wasanii waliotumikia maisha yao katika sanaa.
Dkt Mohammed Gharib Bilal baada ya kumkabidhi Edward Said Tingatinga tuzo ya msanii aliyejitolea maisha yake yote katika sanaa.
Dr Chris Mauki na Jokate Mwegelo walikuwa washehereshaji wa tamasha hilo kwenye Ukumbi wa Mlimani City uliopo Dar es Salaam.
Msanii wa Taarab nchini, Isha Ramadhan 'Isha Mashauzi' akitoa burudani.
Isha Mashauzi akifanya yake na wacheza shoo wake.
Kikundi cha wakina mama kikitoa burudani.
Mc Jokate Mwengelo (kulia) akikata mauno baada ya burudani kumnogea.
Kikundi maalumu kilichoandaliwa kutoa burudani.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' akifanya yake.
...Akicheza na wacheza shoo wake.
...Akicheza ma mashabiki wake.
...Akiimba wimbo wake wa 'Mdogomdogo' mbele ya mashabiki.
Wakiendelea kucheza wimbo wa 'Mdogomdogo'.
Wakiendelea kufanya yao.
Wanamitindo mbalimbali wakipita mbele ya mashabiki.
Wanamitindo kwa pamoja wakipita mbele ya mashabiki.
Wachekeshaji kutoka nchini Kenya wakitoa burudani.
Waimbaji wanaounda kundi la Yamoto Band Aslay, Becka, Bella na Maromboso wakitoa burudani
(PICHA: MUSA MATEJA/GPL)
Post a Comment