LADY JAYDEE AVUNJA MKATABA NA GARDNER
HABARI mpya kutoka kwa mastaa wanaodaiwa kuvunjika kwa ndoa yao, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ na Gardner G. Habash ‘Kaptaini’, inasemekana wamevunja mkataba wa kuendesha Mgahawa wa Nyumbani Lounge uliopo Ada Estate, Kinondoni jijini Dar.
“Walimfuata mmiliki wa jengo, wakamwambia kwamba wanavunja, akawakubalia,” kilinyetisha chanzo makini. Chanzo hicho kilizidi kwenda mbali zaidi na kudai kuwa mgahawa huo kwa sasa unamilikiwa na mzungu.
‘Lady Jaydee’ na Gardner G. Habash ‘Kaptaini’ wakati wakiwa pamoja.
“Mgahawa kwa sasa unamilikiwa na Mzungu mmoja ambaye amenunua baadhi
ya vitendea kazi walivyokuwa wakivitumia na Jaydee amekuwa akimsaidia
mzungu huyo baadhi ya mambo kwa kuwa ni mgeni Bongo ila sasa Nyumbani
Lounge itafunguliwa kwa jina jipya la M.O.G na Jaydee atafanya shoo ya
ufunguzi kama msanii tu,” kilisema chanzo hicho.Baada ya kushibishwa maelezo hayo, mwanahabari wetu alimtafuta Jide bila mafanikio lakini Gardner alipopatikana, alijibu kwa kifupi.
“Siwezi kuzungumza chochote katika suala hilo.”
Jide na Gardner wanadaiwa kutengana na kila mmoja akiishi kivyake lakini wenyewe wamekuwa wakikanusha.

Post a Comment