DIAMOND AMKUBALI PETIT MAN
HESHIMA! Tofauti na ilivyokuwa ikifikiriwa na wengi kwamba hamkubali shemeji yake, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ameonyesha kumkubali shemeji yake Ahmed Hashimu ‘Petit Man’ hadharani.
Shemeji wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ Ahmed Hashimu ‘Petit Man’ akiwa na 'waifu tu bi'.
Hivi karibuni uvumi uliibuka kuwa Diamond hakufurahishwa na kitendo
cha dada’ke kuolewa na Petit ndipo msanii huyo alipoamua kukata
‘vilimilimi’ kwa kusema uvumi huo hauna ukweli katika sherehe yake ya
kuzaliwa iliyofanyika Oktoba 2, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Golden
Jubilee Tower, Posta jijini Dar.“Kwa bahati mbaya dada yangu Esma anaumwa hajafika humu ndani, sasa kwa kuwa sasa hivi ameolewa na mtu ninayemkubali, namuita mumewe, shemeji yangu ninayemkubali, Petit Man aje kula keki badala yake,” alisikika Diamond.

Post a Comment