BABA AMUONDOA MANYIKA SIMBA
Kipa chipukizi wa Simba, Peter Manyika, Manyika Peter.
Na Said Ally
BABA mzazi wa kipa chipukizi wa Simba, Peter Manyika, Manyika Peter, ameweka wazi kuwa anafurahia kuona mwanaye akiwa na maendeleo mazuri lakini akaenda mbele zaidi na kusema kuwa anajipanga kumfanyia mipango baadaye atakapokuwa tayari aende nje ya nchi akacheze soka la kulipwa.
BABA mzazi wa kipa chipukizi wa Simba, Peter Manyika, Manyika Peter, ameweka wazi kuwa anafurahia kuona mwanaye akiwa na maendeleo mazuri lakini akaenda mbele zaidi na kusema kuwa anajipanga kumfanyia mipango baadaye atakapokuwa tayari aende nje ya nchi akacheze soka la kulipwa.
Mzazi huyo ambaye alikuwa kipa maarufu enzi zake akizidakia Yanga,
Sigara na Taifa Stars, amesema kuwa atafurahia zaidi akiona mwanaye
anacheza soka na kufanikiwa zaidi kuliko yeye.
Manyika ambaye mara ya mwisho alikuwa kocha wa makipa katika timu ya
Seeb FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Falme za Kiarabu, alijijengea umaarufu
kutokana na kuwa kipa mwenye mbwembwe awapo langoni huku akivaa kofia,
ameliambia gazeti hili kuwa ana imani kama mwanaye akiendelea kujituma
basi atafika mbali.
Amesisitiza kuwa anachofanya kwa sasa ni kuandaa mipango ya kumfanya
mtoto wake huyo kupiga hatua zaidi kwa kucheza soka la kimataifa ikiwa
ni tofauti na yeye ambaye mimi nilipoishia katika maisha yangu ya soka.
“Unajua japo bado ni mdogo lakini tayari ameanza kuonyesha kuwa ana
kila sifa ya kucheza soka la kimataifa kutokana na mafundisho mbalimbali
niliyokuwa nikimpa kipindi cha nyuma na ambayo anapatiwa na makocha
wake wa sasa,” alisema Manyika baba.
Manyika mdogo amepata umaarufu baada ya kucheza kwa kiwango cha juu
katika mechi dhidi ya Yanga, Jumamosi iliyopita na kuweka rekodi ya kuwa
kipa mdogo zaidi kuwahi kucheza katika mechi ya wapinzani wao, ambapo
kwa sasa ana umri wa miaka 18.
CHANZO: CHAMPIONI IJUMAA

Post a Comment