ad

ad

YANGA SC WAPEWA WIKI MBILI KUWASILISHA RASIMU YA KATIBA TFF



Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeitaka klabu ya Yanga kuwasilisha rasimu ya Katiba waliyoipitisha, kwa kuzingatia kuwa Muhtasari wa kikao cha Mkutano Mkuu wao wa Juni 1 mwaka huu umeainisha baadhi ya marekebisho waliyofanya kwa tulivyowaelekeza.
Yanga wanatakiwa kuwasilisha rasimu hiyo kabla ya Oktoba 5 mwaka huu. Ikiwa itakubaliwa na TFF, itapelekwa kwa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo ili waweze kufanya uchaguzi wa viongozi wao.

No comments

Powered by Blogger.