ad

ad

USIKU WA KIGODORO - 01


Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com
“UKO wapi Lina?”
“Kwa dada, ndiyo tunataka kutoka kwenda saluni my dear.”
“Lina usinitibue, kwa dada saa hizi wakati unajua kanisani tunatakiwa saa nane kamili mchana, sasa uende saluni saa sita hii utamaliza muda gani? Kanisani utakuja saa ngapi na ndoa itafungwa saa ngapi au hutaki tufunge ndoa Lina?”
“Nitamaliza mapema tu.”
Mara Lina akakata simu…
“Khaa! Yaani Lina kanikatia simu mimi? Ana maana gani?” alijiuliza James. Alipopiga tena iliita bila kupokelewa…
“Afadhali isingepatikana ningesema chaji imeisha, sasa hapokei ina maana gani?” James aliendelea kuwaza…
“Lakini hili suala la Lina kutopokea simu au kukata litaisha lini? Maana ni kawaida yake. Tunaweza kuongea akakata au akawa hapokei. Huyo dada yake anayesema ni mkali sana, ukali wake ni kama wa simba? Afadhali tufunge hiyo ndoa ili aondoke kwa dada yake tuone.”
***
“Lina ulikuwa ukiongea na nani kwenye simu?” Semi, mume wa Lina alimuuliza baada ya kumsikia akisema anajiandaa kwenda saluni na yupo kwa dada yake tena akaita my dear…
“Ni yule rafiki yangu, Agnes anataka nimpeleke kwenye bethidei, mimi sitaki. Sasa nimemdanganya kwamba nakwenda saluni, itafika mahali atakata tamaa mwenyewe,” alisema Lina.
“Hapana mke wangu, Agnes ni rafiki yako mkubwa, nenda kwenye bethidei yake kama amekualika,” alishauri Semi.
“Mh! Haya baby, basi itabaidi niende saluni kweli halafu baadaye niende kwenye shughuli.”
“Sawa. Hakuna shida.”
Moyoni Lina alifurahi sana kwani ndicho alichokuwa akikitaka.
Alijiandaa akatoka kawaida, njiani alimpigia simu Agnes…
“Egi, dili limetiki. Shemeji yako ameikubali ile kamba. Kwa hiyo wewe uko wapi sasa?”
“Yaani fanya fasta, njoo saluni mimi nimeshafika Lina. Halafu James kanipigia simu, anasema umemkatia simu, nikamwambia kuna sababu shemeji asiwe na wasiwasi. Hebu mpigie ajue unakuja saluni.”
Lina alimpigia simu James…
“My dear nimeshafika saluni.”
“Sasa kwa nini ulikata simu?”
“Kawaida tu my dear, hakukuwa na kitu. Nilijua umemaliza kuzungumza.”
“Oke, fanya haraka mimi namalizia saluni, niko na bestimani wangu. Wewe umeshampata Agnes?”
“Ndiyo.”
Baada ya James kukata simu, Lina alibaki na mawazo kibao…
“Hivi lakini mimi Lina ni kwa nini nimekubali kuuingia mkenge kama huu? Yaani wanaume wawili, tena wote wa ndoa? Nitaishije nao sasa? Kwanza mume wangu Semi akijua, si atanichinja?”
Moyoni alijuta sana lakini kwa hatua aliyofikia, haikuwa rahisi agomee ndoa. Akapanga kwenda kugomea kanisani wakati wa kuulizwa na mchungaji, yeye ajibu hayuko tayari!
***
Kanisa zima lilitulia, maharusi siku hiyo walikuwa watatu. Moses na Lydia, John na Elizabeth na James na Lina.
Mwanamke mmoja ambaye alihudhuria ndoa ya Lina na Semi alikuwepo, akashangaa kumwona Lina anaolewa tena huku akijua bado yupo na Semi, akashtuka sana.
Kabla Lina hajamaliza kusema, alimkodolea macho Agnes huku akionekana kama anataka kutokwa machozi…
“Kanitumia shilingi laki moja yule kaka,” alisema…
“Kweli?”
“Kabisa.”
“Basi amekupata. Maana utakimbilia wapi?”
“Si umeona?”
Ilifika mahali, Lina alihesabu kwa kichwa akitumia kumbukumbu zake na kubaini kwamba, alishakula shilingi milioni moja na laki mbili za James, akajisikia huruma na aibu ya mwenyewe.
Siku moja ya Jumapili, James alimpigia simu Lina na kumwalika kwa lanchi kwenye Hoteli ya Riki, Lina alikubali mwaliko huo na kuwekeana ahadi ya kukutana saa saba mchana.
***
Kabla ya kwenda, Lina alijiuliza maswali mengi sana…
“Je, ikifika mahali akaniambia ananipenda itakuaje?”
“Je, akiniambia anataka kunioa? Maana anaonekana kama hana mke!”
“Mh! Hivi nilivyokubali kirahisi si anaweza kusema mi malaya, kwa nini sikutia ngumu kidogo?”
“Hivi nilivyovaa atanikubali kweli? Kama nipo rafu, si kwa kutoka kwenda hotelini.”
Saa saba juu ya alama Lina alifika kwenye mlango mkubwa wa hoteli hiyo, akasimama na kupiga simu kwa James…
“Nimefika, niko nje hapa.”
“Ingia, ulizia mapokezi sehemu ya baa.”
“Oke poa.”
Lina alisaidia na mfanyakazi mmoja wa hoteli hiyo hadi kwenye ukumbi wa baa, akamkuta James ameshakaa anakunywa wine…
“Mambo Lina?”
“Poa, habari yako James?”
“Mungu ananisaidia.”
“Oke. Pole kwa shughuli.”
“Pole wewe, mimi leo niliamua kupumzika, kwa hiyo sijafika ofisini kwangu.”
“Da! Hongera zenu nyie mliojiajiri wenyewe, mnaamua tu, leo siendi, leo nakwenda.”
James alicheka kidogo kisha akamwangalia Lina kwa macho matamu yaliyoonesha dhahiri kwamba anampenda, Lina akahisi aibu na kuangalia chini kwa mbali…
“Enhe, mambo mengine?” alianza Lina…
“Mambo mengine poa. Mimi nimeshakuagizia chakula, najua utakipenda. Lakini nisikuchukulea muda mrefu sana. Ni hivi Lina, kusema ule ukweli mimi nina ndoto za kufunga ndoa na wewe.”
Lina alishtuka, akamtumbulia macho kwa muda huku moyo wake ukipitisha mambo kibao. Aliwaza kuhusu siku ya ndoa yao, akawaza wamepata mtoto, akawaza wanavyotembea mitaani kama mke na mume…
“James, mbona itakuwa ngumu sana.”
“Nilitegemea hilo jibu, lakini pia nilijiandaa kwa kutaka kuujua huo ugumu.”
“Ugumu ni ugeni kati yetu, utawezaje kuzungumzia ndoa kabla ya kufahamiana kwa undani kwanza?”
“Hilo lipo automatiki. Nadhani kubwa ni kujua inawezekana au la, ndiyo iingie awamu ya kufahamiana.”
Lina aliwaza sana.
Alijiambia kwamba akisema ameolewa, angemkatisha tamaa kijana wa watu ambaye kwa siku kumi na mbili tu ameshamlambisha shilingi milioni moja na laki mbili…
“Oke, niko tayari James.”
James alinyoosha mkono na kumshika mkono Lina, akamwambia…
“Siku ya leo itaingia kwenye kumbukumbu ya maisha yangu.”
“Hata mimi pia James.”
“Lakini kuna jambo moja la msingi sana Lina. Najua wewe ni msichana mrembo, mzuri, unavutia na unaishi kwenye dunia yenye wanaume. Je, huna mpenzi kweli?”
“Mmmm…kusema ukweli nilikuwa naye, lakini tulitofautiana lugha tukaachana.”
“Lini?”
“Kama miezi miwili iliyopita. Kuanzia hapo nikasema sitaki tena wanaume, najipanga kwanza. Ndiyo maana hata wewe uliponiambia habari za kuoana nilikataa kwanza.”
“Pole sana baby. Unaweza kunieleza kwa ufupi historia ya maisha yako?”
“Mmmh! Kifupi mimi ni mtoto wa mwisho katika familia ya mzee Joseph Ambakucha yenye watoto watano. Nimezaliwa Kijiji cha Kilole, Korogwe Tanga.
“Baada ya kumaliza masomo Shule ya Msingi Kilole nilichaguliwa kwenda Sekondari ya Wasichana palepale Korogwe. Nilipomaliza masomo nilikwenda kusomea usekretari Tabora, nilipomaliza nikapata kazi kwenye ofisi za kununua madini ya mtu binafsi, baadaye ndiyo nikajiunga kwa wale wazungu wako pale.”
“Oke, nimekusoma. Mimi kama unavyojua. Naitwa James Wingawinga Nampapara, nilizaliwa Mpitimbi, Ruvuma. Ni mtoto wa tatu katika familia nikiwa ndiyo mtoto wa tatu mwenyewe. Nilisomea Ruvuma msingi na sekondari, baadaye nikaja Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
“Baada ya kumaliza chuo niliamua kuwa mjasiriliamali na kwa kuanzisha kampuni yangu ya kusafirisha nje vinyago, ndiyo inaniweka mjini.
“Nimebahatika, nimejenga nyumba Mbezi Beach, nimenunua magari matatu, nina kiwanja kingine Mbezi Beach. Uzuri sina haja ya kuwajengea wazazi wangu kwani baba yangu ana uwezo mkubwa na ndiye aliyenipa mtaji wa baishara.”
Lina alibaki ametumbua macho tu. Hakujua apongeze au achukue hatua gani!
Uhusiano wa wawili hao ulianzia hapo.
Kwa siku hiyo walipomaliza kula, Lina aliingia kwenye gari la James aina ya Toyota Land Cruiser V8 mpaka ofisini kwake, wakati anashuka, James aligeukia nyuma akachukua brifkesi na kuiweka kwenye mapaja yake na kutoa shilingi laki tano…
“Zitakusaidia kwa siku kadhaa.”
“Jamani sweet, mbona ninazo?”
“Usijali baby.”

MAMBO NDO KWANZA YAMEANZA ITAENDELEA

No comments

Powered by Blogger.